Pata taarifa kuu
MALAWI-SIASA-USALAMA

Mmoja wa wanaharakati walioitisha maandamano ajisalimisha kwa polisi Malawi

Mwanaharakati wa haki za binadamu na kisiasa nchini Malawi Timothy Mtambo, amejisalisha kwa maafisa wa polisi, siku mbili baada ya maafisa wa usalama  kutoa agizo la kukamatwa kwake.

Wafuasi wa upinzani wakisherehekea uamuzi wa Mahakama ya Katiba wa kubatilisha matokeo ya uchaguzi nchini Malawi ambapo Peter Mutharika aliibuka mshindi, Februari 4, 2020.
Wafuasi wa upinzani wakisherehekea uamuzi wa Mahakama ya Katiba wa kubatilisha matokeo ya uchaguzi nchini Malawi ambapo Peter Mutharika aliibuka mshindi, Februari 4, 2020. REUTERS/Eldson Chagara
Matangazo ya kibiashara

Mtambo yupo mikononi mwa polisi baada ya kuitisha maandamano baadaye mwezi huu.

Anakuwa mwanaharakati wa tatu kukamatwa baada ya wenzake wawili Gift Trapence na  MacDonald Sembereka kukamatwa hivi karibuni.

Wanaharakati hao kwa miezi kadhaa sasa wamekuwa wakiitisha maandamano katika miji mbalimbali nchini humo kushinikiza kujiuzulu kwa maafisa wa Tume ya Uchaguzi baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka uliopita.

Mwezi uliopita, Mahakama ya Katiba nchini Malawi ilifuta matokeo yaliyompa ushindi rais Peter Mutharika na kuagiza kuwa Uchaguzi mpya ufanyike baada ya siku 150.

Bunge nchini humo limepitisha mswada wa kufanyika kwa Uchaguzi huo mpya tarehe 19 mwezi Mei, lakini hadi sasa rais Mutharika ambaye amekata rufaa kuhusu uamuzi huo wa Mahakama ya Katiba, hajatia saini  miuswada huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.