Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi Mkuu kufanyika Agosti 16 Ethiopia

Uchaguzi Mkuu nchini Ethiopia, unatarajiwa kufanyika tarehe 16 mwezi Agosti. Huu utakuwa uchaguzi wa kwanza, chini ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed ambaye baada ya kuchukua madaraka mwaka 2018, amekuwa akiongoza mageuzi ya kisiasa nchini humo.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed. Ebrahim Hamid / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Uchaguzi imetoa tangazo hilo, baada ya kuahirishwa kutoka mwezi Mei.

Waziri Mkuu wa Ethiopia ameeleza kuwa nchi yake inakabiliwa na changamoto nyingi siyo vifaa vya uchaguzi tu, bali kuna changamoto nyingine kama za usalama na amani.

Uchaguzi huo Mkuu unatarajiwa kuwa wa kwanza chini ya uongozi wa mshindi huyo wa tuzo ya Nobel ambaye alichukua wadhifa wa Waziri Mkuu wa Ethiopia Aprili mwaka 2018.

Hivi Karibuni Waziri Mkuu aw Ethiopia aliwataka wananchi wa Ethiopia pamoja na vyama vya siasa vya nchi hiyo kusaidia ili uchaguzi huo ufanyike katika mazingira ya amani na demokrasia.

Tangu alipochukua uongozi nchini Ethiopia, Abiy Ahmed amefanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kisiasa na kumletea sifa kubwa kieneo na kimataifa, ingawa mabadiliko hayo yamepelekea pia kuibuka machafuko katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.