Pata taarifa kuu
ETIOPIA-CRISIS GROUP-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Ripoti: Uchaguzi unaweza kuahirishwa kutokana na joto la kisiasa Ethiopia

Ripoti ya Shirika la Kimataifa la International Crisis Group, inaonesha kuwa machafuko ya kikabila na mvutano wa kisiasa kati ya wanasiasa huenda yakasababisha Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Mei mwaka 2020 kuahirishwa.

Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Ethiopia, wakati wa kikao cha bunge huko Addis Ababa, Oktoba 22, 2019.
Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Ethiopia, wakati wa kikao cha bunge huko Addis Ababa, Oktoba 22, 2019. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Tangu alipoingia madarakani mwaka 2018, Waziri Mkuu Abiy Ahmed amekuwa akikabiliwa na maandamano ya mara kwa mara licha ya kiongozi huyo kuwa na rekodi nzuri ya mageuzi ambayo imemsaidia kupata tuzo ya amani ya Nobel.

Hata hivyo wachambuzi wa siasa wanaona kuwa, Waziri Mkuu Ahmed ataendelea kushinikiza kufanyika kwa uchaguzi huo, kwa lengo la kuondoa maswali kuhusu uhalali wake iwapo atashinda, na baada ya kuvunja muungano uliokuwa unatengeza vyama vya EPRDF na sasa kuwa chama kimoja kinachojulikana kama Prosperity Party.

Daktari Abiy Ahmed anatoka katika kabila kubwa zaidi nchini Ethiopia la Oromo ambalo limekuwa likifanya maandamano ya kuipinga serikali tangu mwaka 2015

Alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa muungano unaotawala EPRDF, hatua iiliyomfanya kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo.

Dkt Ahmed, 43, antazamwa na wengi kama mwenye kuzungumza kwa uwazi, mwenye ujuzi na uzoefu, na mwenye kukumbatia uongozi wa kuwashirikisha wote.

Miaka ya nyuma aliwahi kuhudumu kama waziri na alikuwa na mchango mkubwa katika kuanzisha shirika la ujasusi la taifa hilo.

Abiy alizaliwa Agaro kusini Ethiopia katika eneo la Jima tarehe 15 Agosti 1976 na baba Mwislamu kutoka jamii ya Oromo na mama Mkristo kutoka jamii ya Amhara.

Mfahamu Dkt Abiy Ahmed

Dkt Abiy anaangaliwa kama mwanasiasa mwenye kukubalika ambaye ana siasa ya kuwashirikisha watu katika masuala yanayowahusu, na mwenye mafanikio makubwa upande wa elimu na jeshi.

Ana taaluma ya udaktari katika masuala ya amani na usalama kutoka chuo kikuu cha Addis Ababa na ana shahada ya uzamili ya mabadiliko ya uongozi kutoka Chuo Kikuu cha Greenwich, London Uingereza.

Ana shahada ya uzamifu katika usimamizi (MBA) chuo kikuu cha Ashland Leadstar aliyoipata 2013 baada ya kukamilisha masomo yake ya shahada ya kwanza ya Kompyuta kutoka chuo cha habari cha Microlin mjini Addis Ababa mwaka 2001.

Abiy anazungumza vizuri lugha za Afan Oromo, Amharic na Tigrinya, pamoja na Kiingereza.

Dkt Abiy anaangaliwa kama mwanasiasa mwenye kukubalika ambaye ana siasa ya kuwashirikisha watu katika masuala yanayowahusu, na mwenye mafanikio makubwa upande wa elimu na jeshi.
Dkt Abiy anaangaliwa kama mwanasiasa mwenye kukubalika ambaye ana siasa ya kuwashirikisha watu katika masuala yanayowahusu, na mwenye mafanikio makubwa upande wa elimu na jeshi. Ebrahim Hamid / AFP
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.