Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SIASA

Kura ya maoni yapigwa kwa mustakabali wa Sidima, Ethiopia

Watu wa kabila la Sidama nchini Ethiopia, wanapiga kura ya maoni leo Jumatano kwa lengo la kuunda jimbo lao, suala ambalo wachambuzi wa mambo wanasema linaendelea kuligawa taifa hilo kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Umati wa vijana wa eneo la Sidima mbele ya bango linalowataka raia kupiga kura ya maoni Novemba 20, Hawassa, Ethiopia, Novemba 17, 2019.
Umati wa vijana wa eneo la Sidima mbele ya bango linalowataka raia kupiga kura ya maoni Novemba 20, Hawassa, Ethiopia, Novemba 17, 2019. © REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwezi Julai, kumekuwa na maandamano yaliyosababisha watu zaidiu ya watu 10 kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika makabiliano ya maafisa wa usalama na waandamanaji.

Ethiopia kwa sasa, ina majimbo tisa yanayojitegemea na katiba ya nchi hiyo inaitaka serikali kugharamia kura ya maoni iwapo kiutakuwa na kabila ambalo litataka kuunda jimbo lao.

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anakabiliwa na kibarua kigumu kujaribu kuzuia ukabila ambao unatishia kuongeza mgawanyiko nchini humo.

Kura hiyo ya maoni inaonekana kama jaribio la iwapo hofu kuhusu makabila yanayotaka kujitenga inaweza kutatuliwa kwa amani.

Kwa muda wa siku tisa, zaidi ya wapigakura milioni 2.3 wamejiorodhesha. Mchakato ni rahisi sana, sawa na matokeo yanayotarajiwa kwa hamu na gamu na wakaazi wa eneo hilo.

Wakaazi wa Sidama wanasema kuwa wana imani kuwa eneo lao sasa linataka kujitawala, na hali hiyo itapelekea uchumi kuimarika na kujiendeleza kisiasa na kijamii.

Tangu alipoingia madarakani mwezi Aprili 2018, waziri mkuu Abiy amesifiwa kwa kuleta mabadiliko chungu nzima.

Lakini hatua yake ya jinsi anavyoangazia mashirika na vyama vinavyopigania haki ya makabila tofauti imezua hofu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.