Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SIASA

Ethiopia: Mustakabali wa eneo la Sidama kujulikana hivi karibuni

Watu wa kabila la Sidama nchini Ethiopia, siku ya Jumatano, watapiga kura ya maoni kwa lengo la kuunda jimbo lao, suala ambalo wachambuzi wa mambo wanasema linaendelea kuligawa taifa hilo kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Bendera ya Jimbo la Sidama karibu na bendera ya Ethiopia.
Bendera ya Jimbo la Sidama karibu na bendera ya Ethiopia. © Michael TEWELDE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwezi Julai, kumekuwa na maandamano yaliyosababisha watu zaidiu ya watu 10 kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika makabiliano ya maafisa wa usalama na waandamanaji.

Ethiopia kwa sasa, ina majimbo tisa yanayojitegemea na katiba ya nchi hiyo inaitaka serikali kugharamia kura ya maoni iwapo kiutakuwa na kabila ambalo litataka kuunda jimbo lao.

Kwa muda wa siku tisa, zaidi ya wapigakura milioni 2.3 wamejiorodhesha. Mchakato ni rahisi sana, sawa na matokeo yanayotarajiwa kwa hamu na gamu na wakaazi wa eneo hilo.

Wakaazi wa Sidama wanasema kuwa wana imani kuwa eneo lao sasa linataka kujitawala, na hali hiyo itapelekea uchumi kuimarika na kujiendeleza kisiasa na kijamii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.