Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI

Uchaguzi wa mwaka 2020 wazua mjadala DRC

Takriban dola milioni 130 zimetengwa kufadhili uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2020, lakini hakuna mfadhili yeyote aliyeshirikishwa. hali ambayo imeibua maswali mengi nchini humo.

Makao makuu ya Tume ya Uchaguzi DRC (CENI) Kinshasa, Januari 9, 2019 (picha ya kumbukumbu).
Makao makuu ya Tume ya Uchaguzi DRC (CENI) Kinshasa, Januari 9, 2019 (picha ya kumbukumbu). © REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga Ilunkamba amesema ana imani kuwa watakusanya mapatoya kutosha. Kwa upande wa waangalizi wengi, shughuli za kupiga kura zitahitaji pesa zaidi.

Pamoja na jumla ya dola milioni 130, "haiwezekani" kuandaa uchaguzi, shirika moja linalofuatialia uchaguzi limebaini. Kwa upande wa Abraham Djamba, mratibu wa shirika hilo, amesema muswada huo wa sheria unaonyesha kwamba hakuna "nia ya kisiasa" ya kuandaa uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2020.

Mwaka 2018, Tume ya Uchaguzi (CENI) ilikadiria dola milioni 400 kwa kuandaa uchaguzi wa serikali za mitaa, uchaguzi ambao haukufanyika. Tume ya uchaguzi kwa wakati huu imejizuia kusema kuhusu matumizi ya dola milioni 130. CENI inasema inasubiri sheria ipitishwe ili iweze kujieleza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.