Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Maandamano yaendelea Algeria licha ya ahadi za Bouteflika

Maelfu ya wanafunzi wamendamana kwa mara nyingne tangu mapema mchana Jumanne wiki hii katika mji mkuu Algiers na katika miji kadhaa nchini Algeria dhidi ya muhula wa 5 wa rais Abdelaziz Bouteflika.

Wanafunzi wakiandamana katika mji wa Algiers dhidi ya muhula wa tano wa rais Bouteflika.
Wanafunzi wakiandamana katika mji wa Algiers dhidi ya muhula wa tano wa rais Bouteflika. © REUTERS/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji wenye hasira wamefutilia mbali ahadi za rais Bouteflika kuhusu mageuzi katika serikali na kutomaliza muhula wake mpya.

"Hey Bouteflika, hakutakuwa na muhula wa 5" au "Rejesha makambini kikosi cha jeshi na kikosi cha BRI (kikosi cha palosi ya kuzima ghasia), hakutakuwa na muhula wa 5", wanafunzi wameimba walipokuwa wakiandamana katikati mwa mji mkuu Algiers, huku wakipigiwa makofi na watazamaji au kupigia honi na waendesha magari.

Maelfu ya wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali hvya Oran, mji wa pili kwa waliandamana na kukusanyika katikati mwa mji huo, mwandishi wa habari wa eneo hilo ameliambia shirika la Habari la AFP.

Maelfu ya wanafunzi, wakiongozana na walimu pia wameandamana Constantine, mji wa tatu kwa ukubwa, kwa mujibu wa mwandishi wa habari katika eneo hilo, na huko Annaba, mji wa nne kwa ukubwa, maandamano yanaendelea ambapo mwandishi wa habari katika eneo hilo anasema mandamano hayo yameitikiwa na umati wa watu.

Kwa mujibu wa mkaazi mmoja, aliyehojiwa na shirika la Habari la AFP, maelfu ya wanafunzi pia wanaandamana katika mji wa Bejaia (kilomita 180 kusini mwa Algiers) huko Kabylie.

Wanafunzi wanaandamana kwawingi pia katika miji ya Blida, Bouira na Tizi Ouzou, kwa mujibu wa tovuti ya habari ya TSA na katika miji ya Setif, Tlemcen, kwa mujibu wa tovuti ya gazeti la kila siku la El Watan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.