Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Maelfu ya waandamanaji wamiminika katika mitaa ya miji mikubwa Algeria

Mamia kwa maelfu ya waandamanaji wamefurika leo Ijumaa katika miji mbalimbali nchini Algeria, wakipinga rais Abdelaziz Bouteflika kuwania katika uchaguzi wa urais ujao.

Maandamano dhidi ya muhula wa tano wa Bouteflika Algiers, Februari 26, 2019.
Maandamano dhidi ya muhula wa tano wa Bouteflika Algiers, Februari 26, 2019. © RYAD KRAMDI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Bouteflika, mwenye umri wa miaka 81anaendelea kukabiliwa na maandamano ya watu wenye hasira.

Maandamano haya ambayo yalianzishwa hasa na vijana, hivi karibuni vyama karibu vyote vya upinzani vilijunga na vijana hao na kupinga Abdelaziz Bouteflika kuwania tena muhula wa tano katika uchaguzi ujao.

Tangu wiki iliyopita, karibu vyama vyote vya upinzani vimejiunga na waandamanaji. Wanafunzi pia wamehamasishwa wiki hii, hata waandishi wa habari, ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari vya serikali, ili kupinga udhibiti na shinikizo wanazozipata katika kazi yao.

Mapema wiki hii Waziri Mkuu wa Algeria alitangaza kuwa rais Bouteflika atapeleka fomu yake ya kuwania katika uchaguzi ujao Jumapili Machi 3, tarehe ya mwisho kwa wagombea waliochelewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.