Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Algeria yaendelea kukumbwa na maandamano kupinga muhula wa tano wa Bouteflika

Mamia ya watu wamejitokeza Jumapili usiku wa kuamkia leo Jumatatu katika miji mbalimbali nchini Algeria kupinga muhula wa 5 wa rais Abdelaziz Bouteflika ambae ameahidi kufupisha muhula iwapo atachaguliwa kuwa rais katika uchaguzi mkuu ujao.

Makao makuu ya Baraza la Katiba jijini Algiers, ambapo wagombea kwenye kiti cha urais wamefikisha fomu zao. Muda wa mwisho ulikuwa Jumapili, Machi 3, 2019 usiku wa manane.
Makao makuu ya Baraza la Katiba jijini Algiers, ambapo wagombea kwenye kiti cha urais wamefikisha fomu zao. Muda wa mwisho ulikuwa Jumapili, Machi 3, 2019 usiku wa manane. © REUTERS/Ramzi Boudina
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo ahadi hiyo ya rais Bouteflika haikuwashawishi wananchi ambao usiku katika mji wa Alger walijitokeza kwa wingi na hata katika miji mingine wakiandamana kwa utulivu kbal ya ya polisi kusambabzwa katika maeneo mbalimbali huku Helikopta ikipaa hewani usiku kwa ajili ya ulinzi zaidi.

Mapema jana mchana, Mkurugenzi wa kampeni wa rais Abdelaziz Bouteflika Abdelghani Zaalane aliwasilisha mbele ya Baraza la Kikatiba jijini Algiers fomu ya rais ambae hata hivyo amelazwa hospitalini nchini Uswisi na ambapo haikufahamishwa ni lini atarejea nchini humo.

Raia wa Algeria waishio nchini Ufaransa nao pia wamejitokeza jana kuandamana kupinga kile wanachodai kuongozwa na mtu mgonjwa ambae tayari uwezo wake wa kuongoza umetoweka.

Maandamano mfululizo yameendelea kushuhudiwa nchini Algeria katika siku zote hizi za karibuni, kupinga muhula wa 5 wa rais Bouteflika mwenye umri wa miaka 82 ambae alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1999 na baada ya hapo amekuwa akichaguliwa na kushinda kwa zaidi ya asilimia 80 ya kura katika duru ya kwanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.