Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-ICC-HAKI

Wafuasi wa Gbagbo washangilia uamuzi wa ICC

Mahakama ya Kimataifa ya ICC, imemwachilia huru rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo, aliyekuwa ameshtakiwa kwa madai ya uhalifu wa kivita na makosa mengine baada ya machafuko ya kisiasa yaliyosababisha zaidi ya watu 3,000 kupoteza maisha nchini humo mwaka 2010.

Wafuasi wa Laurent Gbagbo waonyesha furaha yao huko Abidjan baada ya kumachilia huru rais wa zamani wa Cote d'Ivoire, Januari 15, 2019.
Wafuasi wa Laurent Gbagbo waonyesha furaha yao huko Abidjan baada ya kumachilia huru rais wa zamani wa Cote d'Ivoire, Januari 15, 2019. © SIA KAMBOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Kimataifa ya ICC, imemwachilia huru rais wa zamani wa Iviry Coast Laurent Gbagbo, aliyekuwa ameshtakiwa kwa madai ya uhalifu wa kivuta na makosa mengine baada ya machafyuko ya kisiasa yaliyosababisha zaidi ya watu 3,000 kupoteza maisha nchini humo mwaka 2010.

Majaji wa Mahakama hiyo, wakiongozwa na Jaji Cuno Tarfusser amesema, uamuzi huo umefikiwa baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuwalisha ushahidi dhidi ya Gbagbo na msaidizi wake Charles Ble Goude.

Uamuzi huu umeleta furaha kubwa kwa wafausi wa Gbagbo hasa jijini Abidjan, huku ikiwa ni pigo kwa upande wa mashataka.

Laurent Gbagbo na Charles Ble Goude, walikuwa wamezuiwa wakati kesi yao ikiendelea kwa muda wa miaka saba.

Laurent Gbagbo, alikuwa rais wa kwanza duniani kufikishwa na kufunguliwa mashataka katika Mahakama hiyo mjini Hague.

Mzozo wa kisiasa ndio uliompeleka Gbaggo katika Mahakma hiyo, baada ya kuzuka kwa machafuko ya baada ya Uchaguzi mwaka 2010.

Gbagbo alikuwa anapambana na rais wa sasa Alassane Ouattara , ambaye alishinda Uchaguzi huo na kutangazwa na Tume ya Uchaguzi.

Hata hivyo, Mahakama ya Kikatiba, ilimtangaza Gbagbo mshindi wa Uchaguzi huo.

Mzozo huo ulisababisha machafuko ambayo yalisababisha vifi vya zaidii ya elfu tatu, huku makabiliano yakishuhudiwa jijini Abidjan kwa karibu siku 10.

Wakati wa mzozo huo, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Ufaransa walitangaza kumtambua Outtara kama mshindi.

Baadaye, wanajeshi wa Ufaransa kwa msaaDa wa vikosi tiifu kwa outtara, walimkamata Gbagbo kwa nguvu akiwa Ikulu na kumsafirisha kwenda kufunguliwa mashtaka katika Mahkama ya ICC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.