Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-DRC-JOSEPH KABILA

DRC: Taifa tajiri linalodumazwa na mizozo

Nchi ya DRC ni nchi ya pili kwa ukubwa barani Afrika, baada ya Algeria yenye utajiri mkubwa, lakini raia wake bado wanaishi katika umasikini.

Wanajeshi wa serikali katika eneo la Kiwanja, amashariki mwa DRC
Wanajeshi wa serikali katika eneo la Kiwanja, amashariki mwa DRC Reuters
Matangazo ya kibiashara

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imebarikiwa kuwa na utajiri wa madini, ardhi, mito hasa mto Congo na misitu mikubwa.

Takwimu za Benki ya dunia zinaonesha kuwa, mwaka 2017, uchumi wa nchi hiyo ulikuwa kwa asilimia 3.7.

Licha ya utajiri huu, taifa hili la Afrika ya Kati lililopata uhuru wake kutoka kwa Wabelgiji mwaka 1960, wananchi wake wameendelea kuishi kwa umasiki mkubwa.

Miongoni mwa madini yanayopatikana katika taofa hilo lenye zaid ya watu Milioni 80 ni pamoja na Cobalt, fedha na Coltan.

Mbali na madini hayo nchi hiyo pia ina shaba , dhahabu, Almasi, miongoni mwa madini mengine ambayo yamezikwa ardhini lakini kwa muda mrefu sasa, hamegeuka kuwa laani badala ya baraka.

Maeneo yenye utajiri huu, yamegeuka kuwa ngime ya waasi, hasa Mashariki mwa nchi hiyo na kusababisha utovu wa usalama uisio isha, maelfu wamepoteza maisha na wengine kuyakimbia makwao na kusalia wakimbizi katika mataifa jirani.

Mbali na machafuko, ufisadi na uongozi mbaya umechangia pakubwa katika mateso ya raia wa nchi hiyo ambayo inayoorodheswa katika nafasi ya 161 kati ya nchi 180 zenye ufisadi mkubwa nchini gumo kwa mujibu wa Shirika la Transparency International.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.