Pata taarifa kuu
CAMEROON-SIASA-USALAMA

Raia wa Cameroon kupiga kura kumchagua rais mpya Jumapili

Raia wa Cameroon wanatarajia kupiga kura kumchagua rais wao mpya siku ya Jumapili, wakati hali ya wasiwasi inaendelea kutandaa katika maeneo yanayozungumza Kiingereza, Kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Makao makuu ya Tume ya Uchaguzi Cameroon, Elecam.
Makao makuu ya Tume ya Uchaguzi Cameroon, Elecam. Carine Frenk/RFI
Matangazo ya kibiashara

Mpaka sasa haijafahamika ikiwa wakaazi wa maeneo hayo watashiriki uchaguzi au la.

Wakati huo huo Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kufanyika kwa uchaguzi wa urais katika mazingira ya "amani, ya kuaminika na ya umoja".

Guterres amewahimiza raia wa Cameroon kutekeleza haki yao ya kidemokrasia na kuwataka wadau wote husika na mchakato wa uchaguzi kujizuia na vurugu, kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Amewashauri Pia wagombea wote kutatua tatizo lolote lililohusiana na mchakato wa uchaguzi kupitia njia za kisheria na za kikatiba.

Hivi majuzi naibu msemaji wake Farhan Haq alithibitisha kwamba Umoja wa Mataifa UN unatiwa wasiwasi na hali inayoendelea katika majimbo yanayozungumza lugha ya Kingereza nchini Cameroon na madhara ya matukio hayo katika kipindi hiki kuelekea katika uchaguzi mkuu.

Siku ya jumapili wagombea tisa akiwemo rais anayemaliza muda wake Paul Biya watachuana kuwania nafasi ya urais katika mazingira ya kuendelea kudhohofika kwa usalama kaskazini mwa nchi hiyo kufuatia mashambulizi ya kundi la kijihadi la Boko Haram pamoja na mzozo wa kijeshi unaoendelea katika maeneo yanayozungumza lugha ya kingereza wanaodai mjitengo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.