Pata taarifa kuu
CAMEROON-SIASA-USALAMA

Taharuki yaendelea kutanda kusini magharibi mwa Cameroon

Hali ya wasiwasi inashuhudiwa katika maeneo yanayozungumza lugha ya Kiingereza ya kusini magharibi mwa Cameroon, baada ya serikali kutangaza hali ya hatari kwa muda saa 48.

Mji wa Buea, moja ya  meneo yanayozungumza Kiingereza, Aprili 27, 2018.
Mji wa Buea, moja ya meneo yanayozungumza Kiingereza, Aprili 27, 2018. ALEXIS HUGUET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja kwa sababu ya kuendelea kushuhudiwa kwa makabiliano kati ya wanaharakati wanaotaka maeneo hayo kujitenga na wanajeshi wa taifa hilo.

Wanaharakati hao wanaadhimisha mwaka mmoja hivi leo tangu waanze harakati za kutaka kujitenga na nchi yao kuitwa Ambazonia.

Maeneo ya kaskazini magharibi na kusini magharibi mwa Cameroon ni ya wakazi wanaozungumza lugha ya Kiingereza na wanaunda asilimia 20 ya wakazi wote wa nchi hiyo.

Cameroon ilikuwa koloni la Ujerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baada ya Ujerumani kushindwa vita, nchi ikagawiwa kati ya Uingereza na Ufaransa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa kama eneo la kudhaminiwa. Mwaka wa 1960, Wafaransa waliacha Cameroon ikawa nchi huru, na kuungana na sehemu ya kusini ya Cameroon ya Kiingereza mwaka 1961 kuunda Shirikisho la Jamhuri ya Cameroon.
Baadaye jina likabadilishwa kuwa Jamhuri ya Muungano ya Cameroon mwaka wa 1972, halafu tena Jamhuri ya Cameroon (kwa Kifaransa République du Cameroun) mwaka wa 1984.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.