Pata taarifa kuu
CAMEROON-SIASA-USALAMA

Rais wa Cameroon kuzuru maeneo yanayokabiliwa na machafuko

Rais wa Cameroon Paul Biya Jumanne wiki hii anatarajiwa kufanya ziara katika maeneo yanayozungumza Kingereza na ambayo yanakabiliwa na mzozo kufuatia maandamano ya wanaharakati wanaotaka maeneo yao kuwa taifa huru.

RAis wa Cameroon Paul Biya.
RAis wa Cameroon Paul Biya. AFP
Matangazo ya kibiashara

Hali ya wasiwasi ilishuhudiwa Jumatatu wiki hii katika Miji ya Bamenda na Buea kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi mwa Cameroon, maeneo yanayozungumza lugha ya Kiingereza , baada ya serikali kutangaza hali ya hatari kwa muda saa 48.

Hatua hii imekuja kwa sababu ya kuendelea kushuhudiwa kwa makabiliano kati ya wanaharakati wanaotaka maeneo hayo kujitenga na wanajeshi wa taifa hilo.

Jumatatu wiki hii wanaharakati hao waliadhimisha mwaka mmoja tangu waanze harakati za kutaka kujitenga na nchi yao kuitwa Ambazonia. Hali hii inatokea ikiwa zimesalia siku chache kabla ya uchaguzi wa urais.

Wanaharakati wanaodai eneo lao kuwa nchi huru walifaulu kuziteka ofisi za manispaa na kupandisha bendera ya nchi yao.

Amri ya kutotembea usiku imetekelezwa kuanzia Jumapili katika miji ya Buea, Bamenda na Limbe.

Maeneo ya kaskazini magharibi na kusini magharibi mwa Cameroon ni ya wakazi wanaozungumza lugha ya Kiingereza na wanaunda asilimia 20 ya wakazi wote wa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.