Pata taarifa kuu
UFARANSA-NICOLAS SARKOZY

Sarkozy ashtakiwa rasmi kwa rushwa, fedha za Gaddafi zamponza

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amefunguliwa rasmi mashtaka ya rushwa na ufadhili wa kinyume cha sheria wa kampeni kuhusiana na tuhuma kuwa kiongozi wa zamani wa Libya marehemu Kanali Muammar Gaddafi alisaidia kufadhili kampeni zake za urais mwaka 2007.

Nicolas Sarkozy akiwa na marehemu Kanali Muammar Gaddafi alipotembelea Libya tarehe 25 Julai 2007.
Nicolas Sarkozy akiwa na marehemu Kanali Muammar Gaddafi alipotembelea Libya tarehe 25 Julai 2007. REUTERS/Pascal Rossignol
Matangazo ya kibiashara

Baada ya miaka mitano ya uchunguzi na siku mbili za kuhojiwa na polisi akiwa chini ya ulinzi, majaji wanaochunguza kashfa hii kubwa ya kisiasa kuwahi kushuhudiwa nchini Ufaransa waliamua kuwa wanao ushahidi wa kutosha kumshtaki Sarkozy mwenye umri wa miaka 63.

Sarkozy ambaye alihudumu kwa muhula mmoja tu kati ya mwaka 2007 na 2012, alishtakiwa kwa rushwa, ufadhili haramu wa kampeni na kutumia fedha mali ya uma ya Libya, amesema mtoa taarifa mmoja kwenye uchunguzi huo.

Taarifa zinasema kuwa sarkozy aliruhusiwa kurudi nyumbani jana jioni baada ya kumaliza kuhojiwa.

Hata hivyo Sarkozy mwenyewe ameendelea kukanusha mashtaka yanayomkabili na ambayo yamekuwa yakimuandama tangu aondoke madarakani mwaka 2012.

Kiongozi huyu sasa atakuwa na muda wa miezi 6 kukata rufaa dhidi ya mashtaka yanayomkabili, hatua ambayo anatarajiwa kuichukua na majaji watalazimika kufanya uamuzi zaidi kuamua ikiwa wanaushahidi wa kutosha kuendelea na kesi.

Kwa mara ya kwanza alikamatwa na kuhojiwa kwenye kitongoji cha Nanterre magharibu wa jiji la Paris siku ya Jumanne kabla ya kurejea kwa mahojiano mengine siku ya Jumatano.

Tangu mwaka 2013, wachunguzi wamekuwa wakitazama madai yaliyotolewa na watu waliokuwa karibu na Gaddafi akiwemo mtoto wake Seif al-Islam kwamba Sarkozy alichukua fedha hizo mwaka 2007 kwa mtu ambaye alisaidia kumuondoa madarakani miaka minne baadae.

tayari ameshtakiwa katika kesi mbili tofauti zikihusu kughushi risiti za kuonesha alitumia fedha zaidi katika kampeni zake za mwaka 2012 na nyingine inahusu kushirikiana na jaji kula njama.

Chama chake cha Repeblicane kimejotokeza hadharani na kumtetea Sarkozy.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.