Pata taarifa kuu
DRC-UN

DRC: UN yasema watu 47 wameuawa katika kipindi cha mwaka mmoja

Ripoti ya umoja wa Mataifa imeonesha kuwa jumla ya raia 47 wameuawa katika kipindi cha mwaka mmoja wakati vyombo vya usalama vya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo vilipokabiliana na waandamanaji wanaopinga utawala wa rais Joseph Kabila.

Baadhi ya vijana wakiwa wamechoma matairi kwenye moja ya barabara za Kinshasa
Baadhi ya vijana wakiwa wamechoma matairi kwenye moja ya barabara za Kinshasa https://cdn-images
Matangazo ya kibiashara

Sehemu ya ripoti hiyo imedai kuwa kati ya Januari Mosi mwaka 2017 hadi Januari 31 mwaka 2018, watu 47 wakiwemo wanawake na watoto waliuawa na vyombo vya usalama wakati wa maandamano.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa kulikuwa na jaribio lililofanywa na vyombo vya usalama vya DRC kutaka kufunika na kuficha ukweli kuhusu vifo hivi kwa kuondoa miili na kuzuia kazi za waangalizi wa kimataifa.

Ripoti hiyo ilivyochapishwa na mkuu tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa na tume ya umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, Zeid Ra'ad Al Hussein na mjumbe maalumu wa UN Leila Zerrougui wamesema "mauaji na vitendo vingine vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilitekelezwa kutokana na matumizi makubwa ya nguvu yaliyofanywa na vyombo vya usalama dhidi ya waandamanaji."

Umoja wa Mataifa unalaani ukandamizaji wa kupangwa dhidi ya waandamanaji ikiwemo kutumia njia za mateso dhidi ya waandamanaji jambo ambalo linaenda kinyume na sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu pamoja na zile sheria za DRC.

UN imetoa wito wa kuundwa kwa chombo huru kuchunguza vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na vitendo vingine, ukisema ni wazi vyombo vya usalama vimefanya kazi kwa makusudi ya kuficha ukweli.

Zerrougui na Zeid kwa pamoja wameitaka Serikali ya Kinshasa kuruhusu kufanyika kwa maandamano ya amani na watu kutoa maoni kwa uhuru, wakionya matumizi makubwa ya nguvu na kuminya demokrasia kutasababisha vurugu zaidi nchini humo na kutishia maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwishoni mwa mwaka huu.

Maandamano ya uma yameshuhudiwa tangu rais Joseph Kabila akatae kuondoka madarakani baada ya kumaliza muhula wake mwezi Desemba mwaka 2016.

Maandamano matatu makubwa yaliyofanyika tangu wakati huo yamesababisha watu 17 kupoteza maisha.

Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki ambao walisimamia kufikiwa kwa maridhiano ya kisiasa na kukubaliana kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka jana, haukufanyika kwa kile ambacho Serikali na tume ya uchaguzi walidai hawakuwa na fedha za kuandaa uchaguzi.

Kanisa katoliki linataka rais Kabila kuondoka madarakani na kukaa kando wakati wa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 23 mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.