Pata taarifa kuu

Tume ya Uchaguzi DRC kutangaza kalenda ya uchaguzi mwishoni mwa juma

Joto la kisiasa limeendelea kupanda nchini DRC kufuatia Rais Kabila kuendelea kusalia madarakani wakati tayari muda wake ulimalizika tangu mwishoni mwa mwaka 2016.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikky Haley na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi DRC (CENI), Corneille Nangaa, Gombe, Kinshasa, Oktoba 27, 2017.
Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikky Haley na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi DRC (CENI), Corneille Nangaa, Gombe, Kinshasa, Oktoba 27, 2017. REUTERS/Robert Carrubba
Matangazo ya kibiashara

Marekani inapendekeza uchaguzi huo ufanyike mwaka 2018, wakati tayari mwaka 2019 ulikuwa umetajwa na mkuu wa tume huru CENI Corneille Nanga.

Hata hivyo, hivi karibuni, Norbert Basengezi Naibu Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi CENI amesema kalenda ya uchaguzi itatangazwa mwishoni mwa juma hili na mkataba wa Desemba 31 mwaka jana utaheshimiwa na kwamba tayari wamekutana na wajumbe wa taasisi inayofuatilia utekelezwaji wa makubaliano ya Desemba 31 mwaka jana pamoja na wajumbe wa serikali ili kuafikiana kuhusu kalenda hiyo.

Hayo yanajiri wakati shirika moja la kiraia Synergie des Femmes linalowakilishwa na Justine Masika Bihamba likieleza kwamba mashirika ya kiraia yanaweza kuwa na uwezo wa kuliongoza taifa baada ya Rais Kabila na kuutaka Umoja wa Mataifa kuingilia sana katika maswala ya Usalama.

Mgogoro wa kisiasa unaendelea nchini DR Congo, huku maandamano makubwa yakiendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini humo. Mapema wiki hii maandamano makubwa yakumshinikiza Rais Kabila kuaanda ucahguzi mwaka huu yalifanyika katika mji wa Goma, na siku baadae mjini Bukavu mashariki mwa nchi hiyo.

Watu kadhaa wamekamatwa katika maandamano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.