Pata taarifa kuu
DRC

Raia wanne na afisa wa Polisi wauawa Mashariki mwa DRC

Raia wanne na afisa wa Polisi wameuawa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo baada ya kuzuka kwa maandamano kushinikiza kujiuzulu kwa rais Joseph Kabila kufikia mwisho wa mwaka huu.

Rais wa DRC  Joseph Kabila
Rais wa DRC Joseph Kabila REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Mauaji hayo yametokea siku ya Jumatatu mjini Goma, na ripoti zinasema kuwa makabiliano yalizuka kati ya waandamanaji wa utawala bora na demokrasia Lucha.

Afisa huyo wa Polisi alipigwa mawe na waandamanaji waliokuwa na hasira, na kusababisha kifo chake.

Hali ya wasiwasi imeendelea kushuhudia nchini DRC, kutokana na shinikizo za kutaka kufanyika kwa Uchagizi Mkuu mwaka huu kwa mujibu wa mkataba wa kisiasa uliofikiwa mwaka uliopita.

Wapinzani wa rais Kabila, wamekua wakimshutumu kwa kuchelewesha kuandaa uchaguzi lengo la kusalia madarakani.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Balozi wa Mareklani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley, alitembelea Mashariki mwa nchi hiyo na kushinikiza kufanyika kwa Uchaguzi huo kufanyika mwaka ujao.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.