Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA

Shambulizi la majeshi ya serikali laua watu 15 Libya

Watu 15 wakiwemo watoto wameuawa Mashariki mwa Libya, katika shambulizi la angaa lililotekelezwa na jeshi la nchi hiyo katika makabiliano na makundi ya waasi.

Askari wa Libya wakipiga doria karibu na mji wa Sirte Agosti 4, 2017.
Askari wa Libya wakipiga doria karibu na mji wa Sirte Agosti 4, 2017. REUTERS/Ismail Zitouny
Matangazo ya kibiashara

Mji wa Derna umekuwa ukilengwa na wanajeshi wa serikali kwa madai kuwa, unawapa hifadhi makundi ya kigaidi.

Hata baada ya shambulizi hili, jeshi la Libya halijazungumza lolote.

Makandu ya silaha ikiwa ni pamoja na kundi la Islamic State yameendelea kuhatarisaha usalama nchini humo.

Mwishoni mwa mwezi Septemba ndege za kivita za Marekani zilishambulia ngome ya kundi la Islamic State nchini Libya na kusababisha vifo vya wapiganaji 17.

Tangu alipoingia madarakani mwezi Januari, rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akisema jeshi la Marekani litaendelea kupambana na makundi ya kigaidi kote duniani.

Mapigano nchini Libya yamesababisha vifo vya watu wengine na maelfu ya watu kuyahama makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.