Pata taarifa kuu
LIBYA-IS-USALAMA

Ndege za kivita za Marekani zaua wapiganaji 17 wa IS nchini Libya

Ndege za kivita za Marekani zimeshambulia ngome ya kundi la Islamic State nchini Libya na kusababisha vifo vya wapiganaji 17.

Askari wa Libya wakipiga doria karibu na mji wa Syrte ili kuzuia kurudi kwa wapiganaji wa kundi la Islamic State, Agosti 4, 2017 (picha ya zamani).
Askari wa Libya wakipiga doria karibu na mji wa Syrte ili kuzuia kurudi kwa wapiganaji wa kundi la Islamic State, Agosti 4, 2017 (picha ya zamani). REUTERS/Ismail Zitouny
Matangazo ya kibiashara

Ripoti kutoka katika jeshsi la Marekani zinasema kuwa pamoja na mauaji hayo, mashambulizi ya ndege za Marekani yameharibu magari matatu ya wapiganaji hao.

Tangu alipoingia madarakani mwezi Januari, rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akisema jeshi la Marekani litaendelea kupambana na makundi ya kigaidi kote duniani.

Siku ya Jumatano wiki iliyopita askari tisa na raia wawili waliuawa, kilomita 500 kusini mwa Tripoli katika shambulio la wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS).

Askari wasiopungua tisa na raia wawili walikatwa vichwa nchini humo katika shambulio lililodaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State dhidi ya ngome ya majeshi yanayomtii Marshal Khalifa Haftar.

Shambulio hilo lilifanyika mapema alafajiri katika eneo la al-Joufra, kilomita 500 kusini mwa Tripoli, kwa mujibu wa Kanali Ahmed al-Mesmari, msemaji wa kundi la wapiganaji wa NLA linalomtii Marshal Haftar.

Mapigano nchini Libya yamesababisha vifo vya watu wengine na maelfu ya watu kuyahama makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.