Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA

Watu kumi na mmoja wauawa katika shambulio la Daech

Askari tisa na raia wawili waliuawa siku ya Jumatano, kilomita 500 kusini mwa Tripoli katika shambulio la wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS).

Mapigano yanaendelea kurindima Benghazi kati ya vikosi vya Marshal Khalifa Haftar na wapiganaji wa IS.
Mapigano yanaendelea kurindima Benghazi kati ya vikosi vya Marshal Khalifa Haftar na wapiganaji wa IS. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Askari wasiopungua tisa na raia wawili walikatwa vichwa siku ya Jumatano nchini Libya katika shambulio lililodaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State dhidi ya ngome ya majeshi yanayomtii Marshal Khalifa Haftar.

Shambulio hilo lilifanyika mapema alafajiri katika eneo la al-Joufra, kilomita 500 kusini mwa Tripoli, kwa mujibu wa Kanali Ahmed al-Mesmari, msemaji wa kundi la wapiganaji wa NLA linalomtii Marshal Haftar.

Siku ya Jumatano alasiri, kundi la Islamic state lilidai kutekeleza shambulio hilo katika taarifa iliyotolewa na shirika lake la propaganda la Qama. Anadai kuwa aliua na kujeruhiwa "wanamgambo 21 wa Haftar" katika shambulio la "wapiganaji wa IS" kusini mwa al-Joufra.

Wapiganaji wa kundi la NLA walikua walidhibiti eneo hilo mapema mwezi wa Juni.

Lakini mapigano yanaendelea kati ya makambi mawili karibu na wilaya ya Soug al-Hout.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.