Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Waziri Pierre Kangudia akataa kujiuzulu serikalini

Uongozi wa chama cha UNC uliamua kumuondoa mwakilishi wake, Pierre Kangudia, waziri wa bajeti, kwenye serikali ya muungano, lakini Pierre Kangudia amekataa kutii amri ya chama chake.

Kinshasa, mji mkuu wa DRC.
Kinshasa, mji mkuu wa DRC. Wikimedia/Moyogo
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Bajeti alikutana na waandishi wa habari siku ya Jumanne, Oktoba 24 katika ofisi yake. Alisema yeye iko chini ya mamlaka ya Rais Joseph Kabila, ambaye ndio ana majukumu ya kumfuta kazi kama alivyoteuliwa. Upande wa chama cha UNC, kwanafikiria kuwa alichagua kuondoka kwenye chama.

Pierre Kangudia amesema: "mimi nakataa kuridhisha maslahi binafsi ya baadhi ya watu wanaojipenda kwa sababu wanataka kuzusha mgogoro katika serikali ili kudhoofisha wajumbe wa serikali kutoka upinzani".

Bw. Kangudia amesema kwa maelezo haya mafupi: "Uamuzi wa kujiuzulu serikalini uliwasilishwa kwa Rais wa Jamhuri, Mkuu wa Nchi, ambaye aliniteua kwenye nafasi hii Mei 8, 2017, kwa hiyo niko chini ya majukumu yake. Rais pekee ndiye mwenye majukumu ya kunifuta kazi.

Chama cha UNC kinasema kimefikia uamuzi wa kujiondoa serikalini kwa sababu serikali imeshindwa kuonesha nia ya kuheshimu mkataba wa kisiasa, uliotiwa saini mwaka uliopita, kutaka Uchaguzi kufanyika mwisho wa mwaka huu.

Hakuna uhakika juu ya tarehe ya uchaguzi na kutokuwepo kwa kalenda ya uchaguzi: hizi ndio sababu mbili kuu zilizotajwa na chama cha UNC, ambazo zimepelekea kujiodoa serikalini. Chama cha UNC cha Vital Kamerhe kinasema kuwa kimekubali kushiriki serikalini kwa lengo moja tu, lile la kusaidia kuandaa uchaguzi kulingana na mkataba wa Saint-Sylvestre.

Mkataba huu, uliohitimishwa chini ya usuluhishi wa Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC (CENCO), usem auchaguzi unatakiwa kuwa umefanyika hadi Desemba 31, 2017. Hata hivyo, hakuna kitu kinachoonyesha kuwa tarehe hiyo itaheshimishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.