Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-SIASA

MONUSCO yatoa wito wa kuachiwa huru kwa wapinzani zaidi ya 30

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) imetoa wito wa kuachiwa huru mara moja wafuasi wa upinzani waliokamatwa siku ya Jumapili katika mji wa Lubumbashi, kusini mwa DRC.

Mjini Lubumbashi, katika mkoa wa Haut-Katanga, ambapo wafuasi zaidi ya 30 wa muungano wa upinzani waRassemblement walikamatwa.
Mjini Lubumbashi, katika mkoa wa Haut-Katanga, ambapo wafuasi zaidi ya 30 wa muungano wa upinzani waRassemblement walikamatwa. JUNIOR KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi hao wa muungano wa Rassemblement walikamatwa mwishoni mwa wiki mjini Lubumbashi wakihudhuria mkutano wa chama cha siasa cha UDPS.

Maman Sidikou mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, ametaka serikali kuwaachia wafuasi hao wa upinzani.

Wanachama wa vyama vikuu viwili vya Union for Democracy na wenzao wa Social Progress, walikamatwa siku ya Jumapili katika mji wa Lubumbashi, ulioko Kusini mashariki mwa nchi hiyo, baada ya polisi kuvunja mkutano waliokuwa nao.

Serikali ya Kinshasa imepiga marufuku mkutano wa aina yoyote wa kisiasa, pamoja na maandamano ya upinzani.

Muda wa kuhudumu kama rais kisheri wa DRC ulimalizika mwezi Desemba mwaka jana na kuongezwa kufuatia makubaliano yaliyoafikiwa na baadhi ya vyama vya upinzani.

Tume ya uchaguzi nchini humo (CENI), imeeleza kwamba haitakuwa rahisi kuandaa uchaguzi urais, kabla ya mwezi Aprili mwaka ujao wa 2019.

Chama kingine cha upinzani cha Union for the Congolese Nation, kimetishia kujiondoa serikalini, kama uchaguzi utacheleweshwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.