Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-SIASA

Chama cha UNC chajiondoa serikalini DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, chama cha UNC cha Vital Kamerhe, kimemuondoa mwakilishi wake serikalini.

Vital Kamerhe, kiongozi wa chama cha UNC, Desemba 21, 2016.
Vital Kamerhe, kiongozi wa chama cha UNC, Desemba 21, 2016. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Chama cha UNC kinatetea uamuzi wake kwamba serikali ya DRC haikuheshimu makubaliano ya Saint-Sylvestre. Makubaliano yaliyosainiwa mwezi Desemba mwaka jana na ambayo yanaeleza kuwa uchaguzi ungelipaswa kufanyika kabla ya mwisho wa mwaka huu. Kwa uapande wa chama cha UNC, makubaliano haya hayakutekelezwa.

Hakuna uhakika juu ya tarehe ya uchaguzi na kutokuwepo kwa kalenda ya uchaguzi: hizi ndio sababu mbili kuu zilizotajwa na chama cha UNC, ambazo zimepelekea kujiodoa serikalini. Chama cha UNC cha Vital Kamerhe kinasema kuwa kimekubali kushiriki serikalini kwa lengo moja tu, lile la kusaidia kuandaa uchaguzi kulingana na mkataba wa Saint-Sylvestre.

Mkataba huu, uliohitimishwa chini ya usuluhishi wa Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC (CENCO), unasema uchaguzi unatakiwa kuwa umefanyika hadi Desemba 31, 2017. Hata hivyo, hakuna kitu kinachoonyesha kuwa tarehe hiyo itaheshimishwa. Chama cha UNC kiliomba mwakilishi wake serikalini kujiuzulu. "Uongozi wa kitaifa wa chama cha UNC umeamua kumuondoa mjumbe wa wake serikalini, kwa jina la Pierre Kangudia Mbayi, Waziri wa Bajeti ya Serikali. Chama cha UNC kitaendelea kufanya kazi kwa maslahi ya raia wa DR Congo, "almesema Coco Buatsha Ntumba, mmjumbe wa Kamati kuu ya chama cha UNC.

Kulingana na vyanzo mbalimbali, chama cha UNC kiliiandikia barua Waziri Mkuu Bruno Tshibala kumtaarifu uamuzi huo. Lakini hadi Jumatatu jioni, hakuna barua kutoka kwa Waziri Pierre Kangudia, abayo ilikua tayari imepokea katika ofisi ya waziri mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.