Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZUMA-KURA YA SIRI

Zuma bado aungwa mkono na ANC, licha ya kashfa zinazomkabili

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma bado anaendelea kuungwa mkono na chama chake cha ANC. Hayo yameonekana siku ya Jumanne Agosti 8, alipoponea katika kura ya siri ya kutokua na imani naye iliyopigwa na wabunge.

Jacob Zuma na wafuasi wake Agosti 8, 2017.
Jacob Zuma na wafuasi wake Agosti 8, 2017. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Kura zisizopungua ishirini zilikosa ili rais huyo aondolewe imani na wabunge. Endapo kura hizo zingepatikana, rais Zuma nayeshutumiwa rushwa na kudidimiza uchumi wa Afrika Kusini, angelitakiwa kujiuzulu mara moja. Kwa mwaka mmoja sasa chama cha ANC kinakabiliwa na malumbano ya ndani na tayari chama hicho kimesuhudia migawanyiko.

Mnamo mwezi Agosti 2016, chama cha ANC kilipoteza manispaa ya Johannesburg na Pretoria. Hili ni pigo la kihistoria kwa chama tawala nchini Afrika Kusini tangu mwisho wa utawala wa ubaguzi wa rangi.

Chama cha ANC kimejiunga na kuonyesha nguvu kwa ushauri wa viongozi wa kihistoria wa chama hicho kwa harakati za kupambana na ubaguzi wa rangi. "maveterani" wanaendelea kumtaka rais Jacob Zuma, mwaka mmoja saa, kujiuzulu.

Ahmed Kathrada ni miongoni mwa maveterani hao, aliyekua rafiki bora wa Nelson Mandela, alikataa kuwa Jacob Zuma atahudhuria kwenye mazishi.

Mgogoro huu ulichukua maamuzi mengine katika majira ya baridi mwaka 2017. Zuma amshukuru waziri wa fedha Pravin Gordhan, wa Chama cha Kikomunisti, hali ambayo ilisababisha mvutano mkubwa katika muungano wa ya vyama vitatu nchini Afrika Kusini, muungano ambao ulikua ukiundwa, na cham acha ANC, Chama cha Kikomunisti na chama kikuu cha wafanyakazi cha Cosatu. Cosatu pia inamtaka rais Zuma kujiuzulu na kupiga marufu rais Zuma kuhudhuria kwenye mikutano yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.