Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZUMA-KURA YA SIRI

Hatma ya Zuma hatarini baada ya kura ya siri kupitishwa

Wabunge nchini Afrika Kusini wanatazamiwa kupiga kura ya siri wakati wa kuamua kuhusu hoja ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma leo Jumanne. Tayari Spika wa bunge la Afrika Kusini Baleka Mbete ametangaza na kusema kuwa amepitisha itumiwe kura ya siri katika shughuli hiyo.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, akabiliwa na tuhuma mbalimbali.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, akabiliwa na tuhuma mbalimbali. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni vyama vya upinzani viliwasilisha kesi mahakamani wakitaka kura siri itumiwe katika zoezi hilo. Uamuzi uliopitishwa na upinzani mnamo mwezi Machi.

Upinzani uliomba kura hii itumiwe kura siri katika matumaini ya kujiunga na kundi la wabunge kutoka chama tawala cha ANC ambao wanampinga Jacob Zauma.

Kesi hii ilifikishwa kwenye Mahakama ya Katiba, ambayo iliamua kuwa kura hii iwe ya siri.

Awali kiongozi wa kundi la wabunge kutoka chama cha ANC alielezea kwamba ni jambo la "kutofikiria" kuwa wabunge wa chama hicho watapiga kura ya kutokua na imani dhidi ya rais Zuma. "Hali hii itasababisha mgogoro isiyokuwa wa kawaida," ameonya. Chama cha ANC tayari kimechukuliwa hatua za kinidhamu dhidi ya mbunge ambaye ataunga mkono hadharani kura ya siri.

Chama cha Kikomunisti nchini Afrika Kusini ambacho ni mshirika wa kihistoria wa chama cha ANC kimewataka wabunge wake 17 kukataa kura ya kutokuwa na imani dhidi ya rais Zuma ili kutoiadhibu serikali kwa ujumla. Lakini mazungumzo yanapaswa kuanza kuhusu mustakabali wa Jacob Zuma, chama hiki kiliongeza katika taarifa yake.

Kwa upande wa chama cha wafanyakazi cha Cosatu, kilitoa wito kwa wajumbe wake kujiunga katika maandamano ya siku ya Jumatatu na Jumanne mjini Cape Town na Johannesburg ili kumuomba rais Zuma ajiuzulu.

Chama cha ANC kina wabunge 249 kwa jumla ya wabunge 400 wa Bunge la taifa nchini Afrika Kusini. Ikiwa Wabunge 50 kutoka chama cha ANC watakubali kujiunga na upinzani, hakuna shaka kuwa rais Zuma atakua amefikia hatua ya kuondoka mamlakani.

Itafahamika kwamba Jacob Zuma amenusurika mara kadhaa kura ya kotukuwa na imani naye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.