Pata taarifa kuu
Cyril Ramaphosa: Nasikitishwa kutokana na mgawanyiko katika chama cha ANC

Cyril Ramaphosa: Nasikitishwa kutokana na mgawanyiko katika chama cha ANC

Makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amelaani madai ya ufisadi chini ya uongozi wa rais Jacob Zuma. Ramaphosa amesema ufisadi umekigawa chama cha ANC.

Rais wa Afrika Kusini (kushoto), pia kiongozi wa ANC,  akiadhimisha miaka 104 ya kuzaliwa kwa chama chake Januari 9, 2016, akiwa na Makamu wake Rais Cyril Ramaphosa (kulia).
Rais wa Afrika Kusini (kushoto), pia kiongozi wa ANC, akiadhimisha miaka 104 ya kuzaliwa kwa chama chake Januari 9, 2016, akiwa na Makamu wake Rais Cyril Ramaphosa (kulia). REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii inakuja miezi mitatu kuelekea Mkutano Mkuu wa chama hicho kumtafuta kiongozi mpya wa ANC.

Ramaphosa anatarajiwa kupambana na Nkosazana Dlamini-Zuma, kuwania unyekiti wa chama hicho.

Mwezi Desemba mwaka jana Makamu wa rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, alitangaza kwa mara nyingine tena kuwa yuko tayari kumrithi rais Jacob zuma kwenye uongozi wa chama cha ANC. Hivi karibuni, chama cha ANC kitamchagua kiongozi wake, ambaye atakiwakilisha katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2019.

"Niko tayari kukitumikia chama cha ANC," alisema Cyril Ramaphosa Desemba 14, 2016 kwenye redio moja nchini Afrika kusini. Hii ni mara ya pili ndani ya muda wa wiki ambapo Makamu wa rais alisema kuwa tayari kuchukua uongozi wa chama cha ANC (African National Congress).

Cyril Ramaphosa alisema kuwa anaendelea kuyasikiliza matawi mbalimbali ya chama cha ANC, akitangaza kwamba atafurahi kama atapata uungwaji mkono. Kwa kawaida Makamu wa rais anatakiwa kumrithi rais wake, lakini Cyril Ramaphosa anakwenda kwa tahadhari. Anajua kwamba kumrithi ni vigumu, kwa sababu chama cha ANC kimegawanyika kati ya wanaomuunga mkono Jacob Zuma na wale wanaompinga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.