Watu nane wafariki dunia baada ya kukanyagana nchini Senegal
Watu nane wamefariki dunia baada ya mashabiki wa mpira kukanyagana walipokuwa wakishuhudia michuano ya ligi ya kandanda nchini Senegal.
Imechapishwa:
Waziri wa michezo nchini Senegal Matar Ba amesema msichana mdogo ni miongoni mwa waliopoteza maisha huku majeruhi 60 wakiwahishwa hospitali mjini Dakar.
Duru za habari zinasema kwamba mashabiki wa timu mbili za mpira wa miguu walikabiliana baada ya mchuano uliochezewa katika uwanja wa michezo wa Demba Diop stadium, kumalizika.
Ukuta uliporomoka wakati ambapo idadi kubwa ya watu walipokuwa wakiondoka kwa kasi uwanjani.
Serikali imeahidi hatua madhubuti kuchukuliwa ili kuzuia visa kama hivyo kutokea tena nchini Senegali.