Pata taarifa kuu
ZAMBIA

AFCON U20: Senegal kupepetana na Zambia kwenye fainali Machi 12

Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 imefuzu kucheza hatua ya fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana, baada ya kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Guinea, mchezo uliopigwa mjini Ndola, Zambia.

Vijana wa timu ya taifa ya Zambia wenye jesi za Kijani wakiingia uwanjani kwenye moja ya michezo yao mjini Ndola. 2017
Vijana wa timu ya taifa ya Zambia wenye jesi za Kijani wakiingia uwanjani kwenye moja ya michezo yao mjini Ndola. 2017 CAF Media
Matangazo ya kibiashara

Kwa matokeo haya, vijana wa Senegal sasa watacheza hatua ya fainali Machi 12 mwaka huu ambapo watakutana na wenyeji wa michuano ya mwaka huu, timu ya taifa za Zambia.

Senegal itajaribu kwa mara nyingine kushinda taji hili, baada ya kufungwa kwenye hatua ya fainali za mwaka 2015 na timu ya taifa ya Nigeria.

Vijana wa 'Lions cubs of the Teranga" watakuwa kwenye shinikizo kubwa ifikapo Machi 12 wakati wa mchezo na fainali na Zambia, ambapo wanataka angalau kuwafuta machozi mashabiki wao wa soka kwa kuwa hawajawahi kushinda taji hili la michuano mikubwa barani Afrika.

Ili kuweka ahadi ya mchezo wa fainali na Zambia, timu ya taifa ya Senegal chini ya umri wa miaka 20, ilibidi ifanye kazi kubwa kuwaondoa Guinea, ambapo kikosi cha kocha Joseph Koto, pia kilishuhudia kikikosa penalty kuhitimisha ushindi wao mnono.

Kocha Koto amesema "wachezaji wangu walikuwa na presha uwanjani," na ndio maana hata mchezo wenyewe ulikuwa haueleweki nyakati fulani. Penalty tuliyokosa ilitugharimu sana."

Hata hivyo licha ya kupoteza mchezo dhidi ya Senegal, kocha wa Guinea anasema bahati haikuwa kwao na hivyo walihitaji Mungu awe upande wao kama walihitaji kupata ushindi, lakini hata hivyo amesema hawajakata tamaa.

Timu ya vijana ya Guinea licha ya kuondolewa kwenye michuano hii mikubwa barani Afrika kwenye hatua ya nusu fainali, imefuzu kucheza fainali za kombe la dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 zilizopangwa kufanyika Korea Kusini kuanzia Mei 20 mwaka huu hadi Juni 2017.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.