Pata taarifa kuu
GAMBIA-SENEGAL-ECOWAS

Askari wa Senegal waingia nchini Gambia

Askari wa Senegal wameingia nchini Gambia Alhamisi hii, Januari 19, wakati ambapo rais mteule Adama Barrow aliapishwa wakati wa sherehe rasmi katika ofisi za Uubalozi wa Gambia mjini Dakar, nchini Senegal.

Senegal iliteuliwa na ECOWAS ili kuongoza operesheni ya kuingilia kijeshi dhidi Rais Yahya Jammeh.
Senegal iliteuliwa na ECOWAS ili kuongoza operesheni ya kuingilia kijeshi dhidi Rais Yahya Jammeh. AFP
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la Senegal akinukuliwa na shirika la habari la AFP amebaini kwamba askari wa Senegal waliingia katika ardhi ya Gambia.

Katika azimio lililopitishwa kwa kauli moja Ahamisi hii mchana, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliunga mkono jitihada za ECOWAS kushinikiza Rais anayemaliza muda wake Yahya Jammeh kuondoka madarakani.

Wakati huo huo ndege ya jeshi la Nigeria imeanza kuzunguka juu ya anga ya mji mkuu wa Gambia, Banjul, viongozi wa jeshi la Nigeria wamethibitisha

"Ndege yetu ya kijeshikwa sasa ikko juu ya anga la Gambia," Ayodele Famuyiwa, msemaji wa Jeshi la anga Nigeria amelithibitishia shirika la habari la AFP, akiongeza kuwa "wana uwezo wa kushambulia" kama Yahya Jammeh hataachia ngazi.tangazo hilo linakuja wakati ambapo rais aliyechaguliwa Adama Barrow aliapishwa katika ofisi za ubalozi wa Gambia mjini Dakar.

Rais Barrow, amelazimika kuapishwa nje ya nchi yake kutokana na kuhofia usalama wake pamoja na hatua ya rais Yahya Jammeh kukataa kuondoka madarakani, akipinga matokeo ya uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka jana.

Awali kabla ya kuapishwa kwake, wizara ya mambo ya nje ya Senegal ilidai kuwa kiongozi huyo angeapishwa kwenye ardhi ya nchi yake, lakini haikuwa hivyo na sasa rais Barrow amekula kiapo cha utii kwa nchi yake kwenye ubalozi wa Gambia nchini Senegal.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.