Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Muungano wa COSATU wamtaka rais Zuma ajiuzulu

Muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini Afrika Kusini COSATU unamtaka rais Jacob Zuma ajiuzulu.

Rais wa Afrika Kusini  Jacob Zuma akionekana mwenye huzuni
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akionekana mwenye huzuni REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa COSATU Bheki Ntshalintshali amesema rais Zuma sio mtu sahihi wa kuendelea kuongoza taifa hilo.

Shinikizo za kumtaka rais Zuma kujiuzulu zimeendelea kushuhudiwa baada ya kumfuta kazi Waziri wa fedha Pravin Gordhan wiki iliyopita.

COSATU ambao una wanachama Milioni 1 nukta 8 na mshirika wa karibu wa chama tawala ANC, unasisitiza kuwa kinasisitiza kuwa ni sharti Zuma aachie madaraka kutokana na madai ya ufisadi na ripoti za uchumi wa taifa hilo kushuka.

Uchumi wa Afrika Kusini umeonekana kuyumba huku sarafu ya Rand ikishuka thamani baada ya kufutwa kazi kwa Gordhan.

Wanasiasa wa ANC akiwemo Naibu rais Cyril Ramaphosa wamelaani hatua ya rais Zuma, hali ambayo imekigawa chama hicho.

Wakati hayo yakijiri, vyama vya upinzani nchini humo vinapanga kuwasilisha mswada wa kukosa imani na rais Zuma.

Wanasiasa wa upinzani wanadai kuwa rais Zuma alimfuta kazi Bwana Gordhan kwa sababu alikuwa anawazuia watu wake wa karibu kuiba fedha za Umma.

Hata hivyo,vuguvugu la vijana na wanawake katika chama tawala cha ANC kimemtetea rais Zuma na kusema hatua hiyo ni kupambana na ufisadi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.