Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Upinzani nchini Afrika Kusini wapanga kuwasilisha mswada wa kukosa imani na rais Zuma

Spika wa Bunge nchini Afrika Kusini Baleka Mbete, amesema atafikiria na kufanya uamuzi kuhusu ombi la vyama vya upinzani nchini humo kutaka kuwasilisha mswada wa kukosa imani na rais Jacob Zuma.

Vurugu katika bunge la Afrika Kusini katika siku zilizopita
Vurugu katika bunge la Afrika Kusini katika siku zilizopita Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Upinzani unasema huu ndio wakati wa kumwondoa Zuma madarakani baada ya kumfuta kazi Waziri wa Fedha Pravin Gordhan wiki iliyopita, hatua iliyoshutumiwa vikali na hata wabunge na vigogo wa chama tawala cha ANC.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa upinzani nchini humo kuwasilisha mswada kama huu bungeni kujaribu kumwondoa Zuma madarakani kwa madai ya ufisadi lakini hawakufanikiwa kwa sababu ya wabunge wengi wa chama tawala.

Upinzani kwa sasa unaona kuwa, kutokana na uugwaji mkono wa baadhi ya wabunge wa ANC huenda mswada huo ukaungwa mkono na wabunge wengi.

Vyama vya upinzani  vimelaani hatua hii ya rais Zuma na kwa kile madai kuwa Gordhan alikuwa katika mstari wa mbele kupambana na ufisadi na kuwazuia washirika wa rais Zuma kuiba fedha za umma.

Hata hivyo, Zuma na wafuasi wake wamekuwa wakimshutumu Waziri huyo wa zamani kuhusika na maswala ya ufisadi kwa kushirikiana na Familia ya matajiri wa Kihindi ya Guptas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.