Pata taarifa kuu
MAREKANI-NIGERIA-AFRIKA KUSINI-USHIRIKIANO

Trump azungumza kwa simu na Buhari na Zuma

Jumatatu hii Februari 13 Rais wa Marekani amefanya mazungumzo ya simu na Marais wa Nigeria na Afrika Kusini. Mazungumzo kati ya Rais Donald Trump na mwenzake wa Nigeria Muhammadu Buhari yalijikita katika njia za kuboresha ushirikiano katika vita dhidi ya ugaidi.

Rais wa Marekani Donald Trump akifanya mazungumzo ya simu na wenzake wa Nigeria na Afrika Kusini kuhusu kushirikiano.
Rais wa Marekani Donald Trump akifanya mazungumzo ya simu na wenzake wa Nigeria na Afrika Kusini kuhusu kushirikiano. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Rais Buhari ambaye yuko mjini London kwa ajili ya matibabu, alimpongeza Trump kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani.

Trump alimsihi Rais Buhari kuendelea na kazi nzuri anayoifanya na pia kumpongeza kwa jitihada alizofanya za kuokoa wasichana 24 wa Chibok na hatua zinazopigwa na jeshi la Nigeria.

Trump alimhakikishia rais huyo wa Nigeria kuwa Marekani iko tayari kuafikiana na Nigeria kuhusu suala la kuisaidia na silaha ili iweze kukabiliana na ugaidi.

Rais Trump pia amemualika Buhari kwa ziara nchini Marekani.

Baadaye Trump alizungumza kwa simu na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma. Viongozi hao walikubaliana kufanya jitihada za kuboresha zaidi ushirikiano mzuri uliopo kati ya mataifa hayo mawili.

Marais hao walijadili umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja katika masuala kadhaa ya kuhakikisha kuwepo amani barani la Afrika.

Nchini Afrika Kusini inakadiriwa kuwa kuna kampuni 600 za kimarekani na pia ushirikiano mzuri wa kibiashara kati ya mataifa hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.