Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Kiongozi wa harakati za ubaguzi wa rangi Afrika Kusini Ahmed Kathrada afariki dunia

Afrika Kusini inaomboleza kifo cha mwanasiasa mkongwe, mwanaharakati wa ubaguzi wa rangi na aliyekuwa mfungwa wa kisiasa Ahmed Mohamed Kathrada.

Ahmed Kathrada wakati wa uhai wake. Alifariki  dunia Machi 28 2017
Ahmed Kathrada wakati wa uhai wake. Alifariki dunia Machi 28 2017 umelangnews.co.za
Matangazo ya kibiashara

Maarufu kama Kathy, mwanaharakati huyo amefariki dunia akiwa na miaka 87 baada ya kuugua kwa muda mfupi jijini Johannesburg.

Akiwa na miaka 17 kuanzia miaka ya 1950, Kathrada aliondoka shuleni na kuanza kujihusisha na maswala ya uanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi na kupigania haki.

Msimamo wake ulisababisha uongozi wa Afrika Kusini wakati huo kumpa kifungo cha maisha jela katika Gereza la Kisiwa cha Robben mwaka 1964 kwa kujihusisha na kundi la Umkhonto we Sizwe vuguvugu la kupigania haki.

Kifungo hicho kilimkutanisha na wafungwa wengine kama Nelson Mandela, Walter Sisulu, Govan Mbeki, Andrew Mlangeni, Billy Nair, Elias Motsoaledi, na Raymond Mhlaba.

Ahmed Kathrada wakati alipokuwa anazungumza katika mazishi ya Nelson Mandela mwaka 2013
Ahmed Kathrada wakati alipokuwa anazungumza katika mazishi ya Nelson Mandela mwaka 2013 img.bfmtv.com

Baada ya kifungo cha miaka 26, mwaka 1990 aliachiliwa huru na kuchaguliwa kuwa Mbunge kupitia chama chake cha ANC.

Wakati wa uhai wake, aliandika kitabu kuhusu maisha yake na kile alichopitia Gerezani katika harakati za kulikomboa taifa la Afrika Kusini.

Kitabu chake kinafahamika kama No Bread for Mandela- Memoirs of Ahmed Kathrada, Prisoner No. 468/64.

Aliwahi kuwa pia mshauri wa kiongozi wa kwanza mweusi wa taifa hilo Nelson Mandela ambaye alifariki dunia mwaka 2013.

Miaka ya hivi karibuni amekuwa akikosoa uongozi wa serikali pamoja na chama cha ANC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.