Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-NELSON MANDELA

Mkalimani wa lugha ya ishara anayedaiwa kupotosha umma katika kumbukumbu ya Nelson Mandela azua kizaazaa

Serikali ya Afrika Kusini imetakiwa kumchunguza kwa kina Mkalimani wa lugha ya ishara anayedaiwa kupotosha umma kwa kutumia alama za uongo kutafsiri walichokisema viongozi mbalimbali wa dunia wakati wa hotuba zao katika ibada ya kumkumbuka Rais wa kwanza mzalendo wa nchi hiyo Nelson Mandela. Tayari Naibu Waziri anayeshughulikia maswala ya watu wenye ulemavu ameahidi kuwa watafanya uchunguzi ili kubaini ni kwa nini mtu huyo alikuwa na pasi zilizotolewa kwa ajili ya usalama eneo hilo.

www.theguardian.com
Matangazo ya kibiashara

Mkalimani huyo Thamsanqa Dyantyi alionekana jukwaani na kutafsiri kwa alama hotuba zilizotolewa na viongozi mbambali katika uwanja wa FNB mjini Soweto ambao ulitumika kwa kumbukumbu hiyo siku ya jumanne.

Mapema leo alhamisi Bwana Dyantyi amejitokeza mbele ya vyombo vya habari na kuomba radhi kwa madai kuwa alikuwa na matatizo ya kiafya yaliyoathiri utendaji kazi wake.

Wanachama wa jamii ya watu wenye ulemavu wa kusikia na kuongea nchini Afrika Kusini walilalamikia kitendo hicho na kutaka serikali ichukue hatua kali.

Lakini Chama tawala cha ANC kimesema kimekuwa kikimtumia Mkalimani huyo mara kadhaa katika shughuli zake na hajawahi kulalamikiwa kuwa na matatizo ya kiafya wala ubora wa kazi yake.

Taasisi inayotoa elimu ya Kutafsiri lugha za alama ilisema tayari iliishawasilisha malalamiko dhidi ya Bwana Dyantity, lakini ANC haikuchukua hatua zozote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.