Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-NELSON MANDELA

Mwili wa Nelson Mandela wapumzishwa katika nyumba ya milele

Hatimaye mwili wa Rais wa kwanza mzalendo nchini Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela umezikwa leo jumapili katika kijiji cha Qunu mkoa wa Eastern Cape, mazishi hayo yanatamatisha juma moja la maombolezo ya shujaa huyo wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Reuters/SABC TV
Matangazo ya kibiashara

Mandela aliyefariki akiwa na umri wa miaka 95 baada ya kusumbuliwa na maradhi ya mapafu kwa muda mrefu, amepumzishwa kwa amani kwa misingi ya tamaduni na mila za watu wa ukoo wake wa Xhosa aba Thembu.

Watu wapatao 4,500 wakiwemo wawakilishi wa mataifa mbalimbali wamehudhuria mazishi hayo.

Miongoni mwa waliohudhuria shughuli ya leo ni Mwanamfalme wa Uingereza Charles na Mtangazaji maarufu wa Televisheni nchini Marekani Oprah Winfrey.

Akihutubia maelfu ya watu waliofika kuhudhuria mazishi ya Mandela, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amewataka wananchi wake kuendeleza urithi mwema walioachiwa na kiongozi huyo.

Watu mbalimbali waliopata fursa ya kuhutubia waombolezaji wameeleza wasifu wa kiongozi huyo, huku Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akibainisha jinsi uhusiano baina ya Mataifa hayo mawili ulivyoimarishwa na waasisi wa Mataifa hayo, Hayati Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mandela ambao kwa pamoja wanakumbukwa kwa harakati zao katika historia ya ukombozi barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.