Pata taarifa kuu
CAR-USALAMA

Mapigano makali yaibuka katika mji wa Bangui

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, hali ya utulivu ilishuhudiwa Jumanne hii jioni katika mji mkuu wa nchi hiyo baada ya mapiganomakali yaliyoibuka asubuhi kufuatia mauaji ya afisa wa jeshi mwenye cheo cha kanali. Mpaka sasa watu wanane ndio wanajulikana kuwa waliuawa katika mapigano hayo, ikiwa ni pamoja na afisa huyo wa jeshi na watu kadhaa wamejeruhiwa

Askari wa MINUSCA wakipiga doria katika mitaa ya mji wa Bangui.
Askari wa MINUSCA wakipiga doria katika mitaa ya mji wa Bangui. © MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hali hiyo ilianza Jumanne asubuhi baada ya mauaji ya Kanali Martial Mambeka katika hali ya ulipizaji kisasi na mvutano kati ya makabila hasimu, kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo. Wakati ambapo afisa huyo wa jeshi alikua akiendesha gari lake, watu wawili waiokua kwenye pikipiki walimkaribia wakiwa na bundiki na kumpiga risasi pao hapo.

Wakati huo mapigano yaliibuka. Makundi ya watu wenye silaha yanayotoa ulinzi katika mitaa ya 3, 5 na 6 ya mji mkuu Bangui yalimiminika mitaani na kuanza kufyatua risasi kiholela, huku katika kata ya PK5 watu wenye silaha waliweka vizuizi kwenye barabara zinazounganisha kata hiyo na maeneo mengine ya mji wa Bangui .

Kikosi cha askari wa kulinda amani cha Umoja wa Mataifa (MINUSCA) kiliingilia kati haraka iwezekanavyo, lakini mpaka jioni milio ya risasi ilikua ikisikika.

Waziri wa Usalama wa Raia, Jean-Serge Bokassa, alionya kuwa serikali itafanya kilio chini ya uwezo wake ili haki ikitendeka. Kwa mujibu wa watu kadhaa katika eneo hilo, tangu Jumanne saa sita mchana, hakuna raia anayeruhusiwa kuondoa au kuingi katika kata ya PK5.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.