Pata taarifa kuu
CAR-MAREKANI

Wanamgambo watakiwa kuondoka katika shule wanazoshikilia RCA

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika (Minusca) inaagiza makundi ya waasi kuzachiliwa shule wanazozishikilia. Minusca imetishia kuwatoa katika shule hizo kwa kutumia nguvu kama watakataa kufuata agizo hilo.

Askari wa Minusca kutoka Rwanda, mwezi Mei mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Askari wa Minusca kutoka Rwanda, mwezi Mei mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati. AFP PHOTO / PATRICK FORT
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Takriban watoto 10,000 hawataweza kurudi shuleni mwaka huu, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwa sababu shule nyingi zinashikiliwa na wanamgambo.

Watoto wengine hawawezi kwenda shule kutokana na ukosefu wa usalama na ukosefu wa walimu.

Theluthi tatu ya shule nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati zinashikiliwa na makundi ya watu wenye silaha au zimeharibika wakati wa machafuko nchini humo kuanzia mwaka 2013 hadi 20015.

Rais aliyechaguliwa mapema mwaka huu na serikali yake wana na kazi ngumu ya kurejesha mamlaka ya serikali na kufufua uchumi wa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.