Pata taarifa kuu
CAR-BOZIZE

RCA: Jean-Francis Bozize aachiwa huru kwa muda

Nchini Jamhuri ya Afrika (CAR), Jean-Francis Bozizé, mtoto wa Rais wa zamani wa Afrika ya Kati François Bozizé aliyekamatwa Ijumaa Agosti 5 mjini Bangui ameachiwa huru kwa muda kutolewa chini ya udhibiti wa mahakama.

Mtoto wa François Bozize aliondoka mahakamani Agosti 9 chini ya ulinzi wa kikosi cha MINUSCA. Hawa hapa ni askari MINUSCA nchini JAmhuri ya Afrika ya Kati kutoka Senegakatika mitaa wa mjini Bangui Desemba 10, 2015.
Mtoto wa François Bozize aliondoka mahakamani Agosti 9 chini ya ulinzi wa kikosi cha MINUSCA. Hawa hapa ni askari MINUSCA nchini JAmhuri ya Afrika ya Kati kutoka Senegakatika mitaa wa mjini Bangui Desemba 10, 2015. © MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jean-Francis Bozize, chini ya ulinzi wa kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA), baada ya siku nne akiwa kizuizini alifikishwa mahakamani katika mji wa Bangui Jumanne hii Agosti 9 alasiri, kwenye majira ya saa 10:30 saa za nchini JAmhuri ya Afrika ya Kati. Kwa mujibu wa chanzo cha mahakama, Jean-Francis Bozize alifikishwa mahakamni kwa mara ya kwanza ilikumfahamisha mashataka yanayomkabili na kumpa nafasi ya kujieleza.

Lakini Jean-Francis Bozize, hakupendelea kusikilizwa na majaji lakini alitaka kwanza kujadiliana na mawakili wake. "Aliomba kupata muda wa kuandaa utetezi wake, a,esema wakili wake, Jean-Louis Opalegna. Alipewa muda huo kama inavyotakiwa na sheria. Jaji mwandamizi alitoa nafasi hiyo ya kumkubalia muda huo. "

Waziri huyo wa zamani wa Ulinzi wa Taifa aliondoka mahakamani baada ya saa moja, huku akishindikizwa na askari wa kikosi cha Umoja wa Mataifa (MINUSCA), lakini wakati huu yuko huru kwa muda chini ya udhibiti wa mahakama.

Hatua hii imetolewa na mahakam, lakini kwa masharti. Jean-Francis Bozize haruhusiwi kufanya shughuli za aina yoyote ya kichama au kisiasa , haruhusiwi kumiliki silaha, marufuku ya kuondoka katika ardhi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati au kuwafahamisha viongozi kuhusu kujielekeza sehemu yoyote.

Ifahamike kwamba Jean-Francis Bozize anakabiliwa na makosa mengi: mateso, mauaji ya watu walio mikononi mwa vyombo vya dola, ubadhirifu na mauaji mengine, na uhalifu mwingine unaohusiana na uvunjwaji wa haki za binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.