Pata taarifa kuu
DRC

Upinzani nchini DRC washikilia msimamo wa kuandamana September 19

Upande wa upinzani unaounga mkono Serikali nchini nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC umepinga hatua ya kiongozi wa chama cha upinzani cha UDPS Etienne Tshisekedi wa Mulumba ya kuwataka wananchi kutokuunga mkono mazungumzo ya kitaifa yanayotarajiwa kuanza mnamo alhamisi septemba mosi mwaka huu.

Waandamanaji nchini DRC wakiwa na mabango kuunga mkono muungano wa upinzani
Waandamanaji nchini DRC wakiwa na mabango kuunga mkono muungano wa upinzani RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Upande wa Serikali umesema kuwa mazungumzo ya kitaifa yatafanyika kama yalipangwa na kwamba wananchi wa nchi hiyo wanapaswa kupuuza wito wa upinzani wa kugomea mazungumzo ya kitaifa nchini humo kwa kuwa wito huo unalenga kuwagawa.

Tamko lililosainiwa jana na kiongozi wa upinzani Tshisekedi limewataka wananchi kuandamana kuanzia Septemba 19 mbele ya ofisi za tume ya uchaguzi CENI mjini Kinshasa, kwa lengo la kumshinikiza rais Joseph Kabila kuhakikisha anaachia ngazi desemba 20 mwaka huu.

Rubens Mikindo ni Mratibu wa chama cha Upinzani cha UDPS mkoani kivu kaskazini na hapa anazungumza nasi akiwa mjini Kinshaasa na yeye anaona kuwa Rais Kabila anapaswa kufanya mazungumzo na Etienne Tshisekedi wa Mulumba na kuachana na wapinzani wengine ambao si wakweli.

Francois Rubota Masumbuko ni mbunge wa bunge la kitaifa na mkuu wa chama cha MSR chama kinachoendelea kumuunga mkono rais Kabila baada ya mwasisi wa chama hicho Pierre Lumbi kujiunga na upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.