Pata taarifa kuu
MALI-MAUAJI

Mali: Serikali yatangaza siku tatu ya mombolezo ya kitaifa

Baada ya mashambulizi dhidi ya kambi ya kijeshi ya Nampala Jumanne wiki hii katikati mwa Mali, ambapo askari 17 waliuawa, Serikali imetangaza Jumatano Julai 20 maombolezo ya kitaifa ya siku tatu.

Ibrahim Boubacar Keïta ameamua kutangaza hali ya hatari Mali.
Ibrahim Boubacar Keïta ameamua kutangaza hali ya hatari Mali. Pierre Rene-Worms/RFI
Matangazo ya kibiashara

Hali ya hatari pia imewekwa. Rais Ibrahim Boubacar Keita atahudhuria katika sherehe za kutoa heshima kwa wahanga katika mji wa Segou.

Serikali imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa nchini kote na bendera zitapandishwa nusu mlingoti. Tangazo hilo linatolewa siku moja baada ya mashambulizi mabaya katika kambi kuu ya jeshi ya Nampala Jumanne wiki hii. Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta pia alichukua uamuzi wa kuiweka nchi hiyo katika hali ya hatari kwa muda wa siku kumi. Hatua hii itapelekea, amesema msaidizi wa wa rais Ibrahim Boubacar Keita, kuchukua haraka taratibu zinazoeleweka katika nchi nzima ya Mali kwakuhakikisha usalama wa Mali na raia wake.

Na kwa kutoa heshima kwa askari waliouawa, Rais IBK ameamua kusafiri katika mji wa Segou, kilomita 240 kaskazini mwa mji wa Bamako. Ni mji mkuu wa mkoa wa huo aambapo inapatikana kambi ya jeshi ya Nampala. Katika ziara hiyo pia, Rais IBK atawatembelea askari waliojeruhiwa au wanaolazwa hospitalini.

→ SOMA ZAIDI: Shambulizi la Nampala: Serikali mbioni kujibu

Hali ya utulivu imerejea katika mji wa Nampala Nampala. Hata hivyo bado wakazi wa mji huo wana wasi wasi ya kutokea kwa mashambulizi mengine iwapo serikali haitokua makini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.