Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Kundi la waasi wa Peul ladai kushambulia kambi ya jeshi katikati mwa Mali

Nchini Mali, watu wenye silaha wameshambulia mapema Jumanne asubuhi kambi kuu ya kijeshi ya mjini Nampala. Watu hao walichukua udhibiti wa kambi hiyoinayopatikana katikati mwa nchi karibu na mpaka na Mauritania na zaidi ya kilomita 500 kutoka mji wa Bamako, mji mkuu wa nchi ya Mali.

Kambi ya jeshi la Mali imeshambuliwa katika mji wa Nampala kilomita 400 kaskazini mashariki mwa mji wa Bamako, karibu na mpaka wa Mauritania.
Kambi ya jeshi la Mali imeshambuliwa katika mji wa Nampala kilomita 400 kaskazini mashariki mwa mji wa Bamako, karibu na mpaka wa Mauritania. Β© (Carte : RFI)
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na serikali ya Mali, askari kumi na mmoja wameuawa katika shambulio hilo.

Yote yalianza mapema Jumanne asubuhi. Watu wenye silaha za kivita walishambulia kambi kuu ya mjini Nampala kusini mwa mji wa Bamako. Hii ni kambi muhimu ya jeshi la Mali na washambuliaji, kwa mujibu wa mashahidi, walikua na magari yaliyojaa vifaa vya kijeshi.

Baada ya mapigano ya muda mrefu, walichukua udhibiti wa kambi hiyo na kupandisha bendera nyeusi. Kisha waliwasha moto na mashahidi walikua wakiona wakiwa mbali na kambi hiyo. Moshi mkubwa ulikua ukitokea katika kambi hiyo Jumanne hii.

Kutoka kilomita 80 na mji wa Nampala, katika kijiji cha Niono, mashahidi waliona magari ya wagonjwa yakibeba askari wa Mali waliojeruhiwa.

Sidi CissΓ©, Rais wa muungano kwa ajili ya kuhifadhi utambulisho wa jamii ya Peul, amedai kuwa kundi lake ndio limehusika na uvamizi huo. Kundi hili lilianzishwa muda si mrefu, lakini kinachoeleweka ni kwamba shirika kuu la masuala ya utamaduni ya jamii ya Peul kutoka Mali, Tabital Pulaaku, amesema kuwa hawalitambui kundi hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.