Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mali: uchunguzi baada ya makabiliano makali Gao

Kaskazini mwa Mali, vijana zaidi ya mia moja wamekusanyika Jumatano hii, Julai 13 mbele ya makao makuu ya jimbo la Gao, licha ya ghasia za Jumanne wiki hii. Makabiliano na vikosi vya usalama yalisababisha watu watatu kupoteza maisha na zaidi ya 30 kujeruhiwa.

Kwa uchache watu watatu waliuawa siku ya Jumanne katika jimbo la Gao, kaskazini mwa Mali, wakati wa maandamano ya vijana ya kulaani kuundwa kwa taasisi za mpito katika majimbo matano. Gao, Julai 12, 2016.
Kwa uchache watu watatu waliuawa siku ya Jumanne katika jimbo la Gao, kaskazini mwa Mali, wakati wa maandamano ya vijana ya kulaani kuundwa kwa taasisi za mpito katika majimbo matano. Gao, Julai 12, 2016. REUTERS/Souleymane Ag Anara
Matangazo ya kibiashara

Vijana wa mji wa Gao wanapinga dhidi ya kuanzishwa kwa taasisi za mpito katika mfumo wa mkataba wa Amani ulioafikia mjini Algiers. Jumatano hii asubuhi, mvutano uliibuka kati ya vikosi vya usalama na vijana waandamanaji, lakini vijana bado wako mitaani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari katika mji wa Gao, vijana zaidi ya mia moja walikuwa wakikabiliana mchana huu na vikosi vya usalam karibu makao makuu ya jimbo la Gao. Milio ya risasi imesikika. Hata hivyo hakuna uhusiano wowote na mvutano wa Jumanne Julai 12. Kama baadhi ya maduka yameeendelea kufungwa katika maeneo ya jirani, hali ni shwari katika maeneo mengine ya mji, kwa mujibu wa mashahidi.

Jumanne usiku, vijana wengi ambao walikamatwa waliachiwa baada ya majadiliano kati ya mashirika ya kiraia na viongozi wa jimbo la Gao. Vijana wanaomba kuondoka kwa mkuu wa polisi wa mkoa wa Gao, Seydou Traoré, ambaye, kwa mujibu wa vijana hao, alitoa amri ya kufyatua risasi katika umati wa watu. Seydou Traoré, kwa upande wake, amehusisha vurugu hizo kwa makundi ya watu wenye silaha.

Serikali ya Mali, kwa upande wake, imetangaza kuanzisha uchunguzi ili kutoa mwanga juu ya matukio hayo. Ujumbe wa mawaziri kadhaa, ikiwa ni pamoja Waziri wa Usalama wa Ndanii, wako njiani wakielekea katika jimbo la Gao kukutana na pande mbalimbali.

Vijana wameahidi kuendelea na maandamano ili kupinga dhidi ya kuanzishwa kwa taasisi za mpito. Taasisi hizo zitachukua nafasi ya serikali za mitaa za sasa na zitapelekwa kuanzia Ijumaa Julai 15 katika mikoa mitano ya utawala wa kaskazini mwa Mali, kwa mujibu wa mkataba wa amani uliosainiwa mwaka 2015 na serikali ya Mali na makundi ya waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.