Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

DRC yapuuza Marekani kufungia akaunti za afisa wa polisi

Serikali ya Congo Kinshasa imetupilia mbali hatua ya Marekani kuzuia akaunti za afisa wa jeshi la polisi Celesten Kanyama,kwa mujibu wa msemaji wa serikali Lambert Mende ni kama kuingilia kati masuala ya serikali ya Congo wakati DRC ni nchi huru yenye kujitawala.

Msemaji wa serikali ya Kinshasa Lambert Mende
Msemaji wa serikali ya Kinshasa Lambert Mende FEDERICO SCOPPA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya serikali ya DRC inakuja kufuatia Serikali ya Marekani kutangaza vikwazo dhidi ya afisa mkuu wa jeshi la polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Jenerali Célestin Kanyama aliyeko jijini Kinshasa kufuatia kile inasema amehusika na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu, mauaji pamoja na machafuko jijini humo.

Hayo yanajiri wakati huu kukiwa na idadi kadhaa ya watu wanaodaiwa kutoweka katika mazingira tatanishi ikiongezeka.

Juma hili ripoti ya mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini humo imesema tangu mwezi wa Desemba mwaka jana hadi sasa, utawala wa DRCongo umekuwa ukijihusisha na kamatakamata ya wapinzani na kuzuia kwa nguvu mikusanyiko ya kisiasa ili kukwepa kufanyika kwa uchaguzi kama inavyoagizwa na katiba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.