Pata taarifa kuu
ZIKA-WHO-AMERIKA

WHO hii leo kuamua iwapo ugonjwa wa Zika utangazwe kama hali ya dharura kidunia

Kamati maalumu ya dharura ya shirika la afya duniani WHO, inakutana mjini Geneva, kujadiliana na kuamua iwapo shirika hilo liutangazae ugonjwa wa virusi vya Zika ambao umesababisha madhara makubwa ya watoto wanaozaliwa kwenye nchi za Amerika, kama hali ya dharura kidunia.

Wataalamu wa afya wakipuliza dawa mjini, Buenos Aires, Brazil kudhibiti mbu wanaoambukiza virusi vya Zika 29 janvier 2016.
Wataalamu wa afya wakipuliza dawa mjini, Buenos Aires, Brazil kudhibiti mbu wanaoambukiza virusi vya Zika 29 janvier 2016. REUTERS/Enrique Marcarian
Matangazo ya kibiashara

WHI ilionya juma lililopita kuwa, virusi hivyo wanavyoambukizwa na mbu, vimeanza kuenea kwenye maeneo mengi ya nchi za Amerika, na kwamba nchi hizo zinatarajia kushuhudia zaidi ya wagonjwa milioni nne kwa mwaka huu peke yake.

Shirika la afya liko kwenye shinikizo kubwa la kuchukua hatua za haraka kuhusu virusi vya ugonjwa wa Zika, baada ya kukiri kuwa shirika hilo lilikuwa taratibu sana katika kushughulikia janga la virusi vya Ebola kwenye nchi za Afrika magharibi.

Dispersion de fumigère à Buenos Aires pour tenter d'éliminer les moustiques porteurs du virus Zika, le 29 janvier 2016.
Dispersion de fumigère à Buenos Aires pour tenter d'éliminer les moustiques porteurs du virus Zika, le 29 janvier 2016. REUTERS/Enrique Marcarian

Licha ya dalili za virusi hivi kutoonekana kwa haraka wala kuwa na madhara ya moja kwa moja, inaaminika kuwa virusi hivi kwa sehemu kubwa vinasababisha watoto wanaozaliwa kuwa na matatizo ikiwa ni pamoja na kuzaliwa na vichwa vidogo na ubongo mdogo.

Japokuwa wataalamu wanaendelea na uchunguzi zaidi kuthibitisha ikiwa watoto wanaozaliwa na vichwa vidogo kumetokana na maambukizi ya virusi vya Zika, mkuu wa shirika hilo, Margaret Chan ameonya kuwa kuna uhusiano wa karibu sana.

Virusi hivi vya Zika pia vinahusishwa na magonjwa mengine ya mishipa ya fahamu unaofahamika kama Guillain-Barre Syndrome.

Virusi vya Zika
Virusi vya Zika REUTERS/CDC/Cynthia Goldsmith/Handout

Nchi ya Brazil ilikuwa taifa la kwanza kwenye ukanda wa bara la Amerika kuripoti kesi za ugonjwa huo na kutaka kuchukuliwa kwa hatua za haraka kudhibiti maambukizi zaidi.

Toka wakati huo kumeripotiwa zaidi ya kesi 270 za ugonjwa huu unaofahamika kitaalamu kama Microcephaly, huku watu wengine elfu 3 na 448 wakiripotiwa kuwa na maambukizi.

Hali hii imesababisha nchi za Colombia, Ecuador, El Salvador, Jamaica na Puerto Riko kuwaonya wanawake nchini humo kutopata mimba wakati huu mpaka pale maambukizi ya virusi hivi yatakapodhibitiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.