Pata taarifa kuu
CAMEROON-BOKO HARAM-SHAMBULIO-USALAMA

Cameroon: watu 13 wauawa katika shambulio Msikitini

Shambulio jipya limetokea Jumatano hii asubuhi katika Msikiti wa Kuyape, kaskazini mwa Cameroon. Vyanzo vya usalama vinabaini kwamba watu 11 wameuawa katika shambulio hilo la kujitoa mhanga na mwengine 1 amejeruhiwa.

Vyanzo vya usalama vimebaini kwamba watu 13 wameuawa na mmoja amejeruhiwa katika shambulio hii lilitokea Jumatano hii, Januari 13, kaskazini mwa Cameroon.
Vyanzo vya usalama vimebaini kwamba watu 13 wameuawa na mmoja amejeruhiwa katika shambulio hii lilitokea Jumatano hii, Januari 13, kaskazini mwa Cameroon. © Reinnier KAZE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limetokea katika Msikiti, kaskazini mwa Cameroon, uliokua ukilengwa mara kwa marana wapiganaji kundi la Islamic State katika Afrika Magharibi (Boko Haram).

Kundi la wanamgambo wa kiislam wa Boko Haram la Nigeria limekua likifanya mashambulizi katika nchi jirani za Cameroon, Chad na Niger tangu mwaka jana.
Inaarifiwa kuwa mshambuliaji wa kujitoa mhanga alikuwa akishiriki ibada pamoja na waumini wengine wakati alipojilipua, duru za usalama zimeliambia shirika la habari la AFP.

Shambulio hili la bomu limekuja baada ya watu wawili kuuawa wakati wa usiku katika eneo hilo la Musikiti katika shambulio lingine linaloaminiwa kutekelezwa na Boko Haram, kwa mujibu wa duru za usalama zilizokaririwa na AFP.

Wapiganaji kutoka Nigeria wa kundi la Boko Haram wamekua wakiendesha mashambulizi upande wapili wa mpaka kaskazini mwa Cameroon.

Kampeni ya kundi hilo ya kuanzisha taifa la kiislam kaskazini mwa Nigeria imewauwa watu takriban 17,000 na kuwaacha wengine wapatao milioni tatu bila makazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.