Pata taarifa kuu
UNICEF-BOKO HARAM-USALAMA

UNICEF yainyooshea kidole cha lawama Boko Haram

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulkia maswala ya watoto UNICEF linasema watoto zaidi ya Laki tano wamelazimika kukimbia makwao kutokana na mashambulizi ya kundi la kigaidi la Boko Haram Kaskazini mwa Nigeria na nchi jirani.

Maandamano ya kudai kuachiliwa huru kwa wasichana wadogo waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram katika mji wa Chibok.
Maandamano ya kudai kuachiliwa huru kwa wasichana wadogo waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram katika mji wa Chibok. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo linasema Nigeria ndio inayoathiriwa zaidi na idaidi kubw a ya watoto hao waliokimbia na wazazi wao ni wale wenye umri chini ya miaka mitano.

Watoto wengine zaidi la Lakini Mbli na elfu sitini wameathiriwa na mashambulizi hayo ya Boko Haramu katika jirani za Cameroon, Chad na Niger.

Pamoja na kukosa makaazi watoto hao pia wamwelazimishwa na wpaiganaji hao kujiunga na kundi hilo na kutumiwa kubeba mabomu.

Kundi la Boko Haram limeendelea kuitesa serikali ya Nigeria na tangu mwaka 2009 watu elfu 15 wamepoteza maisha.

Serikali ya rais Muhamadu Buhari pia inaendelea kuwatauta zaiid ya wasichana 200 waliotekwa mwaka jana katika kijiji cha Chibok Kaskazini mwa nchi ambao hadi sasa hawajulikani waliko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.