Pata taarifa kuu
CHAD-BOKO HARAM-MASHAMBULIZI-USALAMA

Chad: mashambulizi matatu ya Boko Haram yawaua watu 37

Mashambulizi matatu yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la Boko Haram yamewaua watu 37 Jumamosi mchana Oktoba 10 katika mji wa Baga Sola, unaopatikana karibu ba mpaka na Nigeria katika mwambao wa Ziwa Chad.

Wanajeshi wa Chad wakipiga doria katika kijiji cha Malam Fatori,  Chad, Aprili 3, 2015
Wanajeshi wa Chad wakipiga doria katika kijiji cha Malam Fatori, Chad, Aprili 3, 2015 AFP/AFP/Archive
Matangazo ya kibiashara

Vyanzo vya kuaminika vimebaini kwamba watu "37 wameuawa na 52 kwamejeruhiwa," kulingana na ripoti ya awali. Mlipuko wa kwanza umetokea katika soko la samaki la Baga Sola na mashambulio mawili mengine yametoke katika kambi ya wakimbizi nje kidogo ya mji.

Milipuko, ambayo imetokea saa 10:00 (sawa na saa 11 saa za Afrika ya Kati), umehusishwa mara moja na kundi la kiislam kutoka Nigeria la Boko Haram, kwa mujibu wa vyanzo vya usalama.

Boko Haram imepenya na kuingia katika mwambao wa Ziwa Chad

Ziwa Chad linagawa Nigeria, Niger, Cameroon na Chad. Ingawa ukubwa wake hupunguzwa kutoka mwaka hadi mwaka kwa sababu ya ongezeko la joto duniani, Ziwa Chad lina wingi wa visiwa na vyenye wavuvi wengi na maeneo ya pembezoni mwa ziwa hilo yanakabiliwa na hali ngumu ya mazingiramisitu mikubwa, ambayo inawezesha wapiganaji wa Boko Haram kupenya kutoka Nigeriana kuingia nchini Chad kufanya mashambulizi. Mwezi Machi, kundi hilo liliendesha mashambulizi katika vijiji kadhaa vya Ziwa Chad, na kuua watu 19. Majira haya ya joto, wapiganaji wa Boko Haram waliendesha mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga katika soko la N'Djamena, mji mkuu wa Chad, na kusababisha vifo vya watu kumi.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, jeshi la Chad linashiriki katika operesheni ya kijeshi za Ukanda huo dhidi ya Boko Haram, ambapo mabomu na mashambulizi vimeenea zaidi kaskazini mashariki mwa Nigeria, ngome ya kihistoria ya Boko Haram, kwa nchi jirani, Chad, Niger na Cameroon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.