Pata taarifa kuu
AU-BURUNDI-MACHAFUKO-USALAMA-SIASA

Rais wa Benin atazamiwa kufanya ziara ya kikazi Burundi

Rais wa Benin anatazamiwa kuwasili mjini Bujumbura, nchini Burundi Jumatatu mchana, Desemba 7 kukutana na Rais Pierre Nkurunziza kuhusu mgogoro unaoikumba nchi hiyo kwa zaidi ya miezi minane sasa.

Rais wa Benin, Thomas Boni Yayi , atumwa na Umoja wa afrika Burundi.
Rais wa Benin, Thomas Boni Yayi , atumwa na Umoja wa afrika Burundi. © AFP PHOTO / POOL / MUJAHID SAFODIEN
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa wamepitisha maazimio ya kuhamasisha serikali na upinzani unaopinga muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza, kukaa kwenye meza ya mazungumzo. Rais wa Uganda amekua tayari kuandaa mazungumzo. Lakini kutokana na ukosefu wa matokeo, Umoja wa Afrika umemuomba rais wa Benin kujaribu kuvunja hali hii inayoendelea kushuhudiwa nchini Burundi.

Ujumbe wa Boni Yayi ulishtukizwa wakati wa mkutano kati ya China na Afrika mjini Johannesburg, nchini Afrika Kusini. Jumamosi Desemba 5, rais wa Tume ya Umoja wa Afrika Nkossazana Dlamini-Zuma amemuomba Rais Boni Yayi kwenda haraka iwezekanavyo nchini Burundi.

"Boni Yayi anazungumza Kifaransa, ameshajadili masuala mengi yanayolikabili bara la Afrika. Nkurunziza na Boni Yayi wote ni wainjilisti", chanzo kilio karibu ya rais wa Benin kimebaini.

Mpango huu hauna nia kwa sasa wa kuchukua nafasi ya rais wa Uganda, ambaye anajianda kuanzisha mazungumzo kwa niaba ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Nchi.

"Sote tunakerwa na hali inayoendelea kushuhudiwa Burundi", chanzo hicho kimeongeza, pia kikibaini kwamba mpango huu unaungwa mkono na mabalozi wengi kutoka nchi za Magharibi.

Rais wa Burundi anasisitiza mazungumzo baina ya Warundi nchini Burundi yakiongozwa na mamlaka tawala, ili waweze kuwa na muda wa kutoa utaratibu wa mazungumzo, orodha ya washiriki na hivyo mahali mazungumzo hayo yatafanyika, jambo ambalo linapingwa na upinzani, wakati ambapo maiti zinaendelea kuokotwa kila kukicha kufuatia mashambulizi ya usiku kati ya wafuasi wa utawala na wale wa upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.