Pata taarifa kuu
AU-BURUNDI-UPATANISHI-SIASA-USALAMA

Mgogoro Burundi: ziara ya rais wa Benin yafutwa

Ujumbe wa rais wa Benin nchini Burundi umefutwa. Kwa mujibu wa wasaidizi wake, rais wa Tume ya Umoja wa Afrika alimtaka kufanya safari ya kusaidia nchi hiyo kuondokana na mgogoro ambao inaendelea kushuhudia tangu kupingwa muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza. Lakini hatimaye, rais wa Burundi hakua tayari kumpokea.

Thomas Boni Yayi, rais wa Benin, alikua anatarajiwa kuwasili Burundi, lakini zaira yake imefutwa katika dakika za mwisho.
Thomas Boni Yayi, rais wa Benin, alikua anatarajiwa kuwasili Burundi, lakini zaira yake imefutwa katika dakika za mwisho. © AFP PHOTO / BERTRAND GUAY
Matangazo ya kibiashara

Ruhusa ya kupita kwenye anga ya Burundi na kutua nchini humo imefutwa, wasaidizi wa Rais wa Benin wamebaini. Rais wa Burundi ameelezea kutokua na muda wa kumpkea rais mwenzake.

Mamlaka nchini Burundi ilikuwa ilisahihisha kanuni ya mkutano kati ya marais wawili mjini Bujumbura, chanzo chetu kimeshangaa. Rais wa Burundi alisikia lengo la ziara ya rais wa Benin nchini mwake na kuwa ziara hiyo ilikua ya kushtukiza, mshirika wa karibu wa Pierre Nkurunziza ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema.

"Mataifa ya Afrika Mashariki yamechukulia vibaya jitihada hii", chanzo katika Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika kimeongeza. Uganda imekabidhiwa na Ukanda suala la Burundi na inaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa ili kuendesha upatanishi kati ya pande zinazohusika katika mgogoro nchini Burundi.

"Lakini ziara ya Boni Yayi kwa vyovyote vile haikua na ujumbe sambamba na ule wa jumuiya ya Afrika Mashariki. Nkosazana Dlamini-Zuma alimpongeza rais wa Uganda kwa jitihada zake za kupatanisha Warundi zinazoendelea", ameeleza mwanadiplomasia wa Benin, ambaye bado ana matumaini kwamba mkutano utafanyika hivi karibuni. Kwa sasa, hakuna tarehe nyingine ya mkutano kati ya viongozi hao wawili iliyotangazwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.